Main Title

source : abna.ir
Jumatano

9 Desemba 2015

17:17:33
723910

Magufuli aongoza Watanzania kusherehekea Uhuru kwa kufanya usafi + Picha

Rais John Magufuli na rais msataafu Dk Jakaya Kikwete nao wamejumuika sanjari na wananchi katika zoezi la kuadhimisha uhuru wa Tanganyika kwa kufanya Usafi nchi nzima.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.

Mamia ya watu walijidamka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.

Rais John Magufuli na rais msataafu Dk Jakaya Kikwete nao wamejumuika sanjari na wananchi katika zoezi la kuadhimisha uhuru wa Tanganyika kwa kufanya Usafi nchi nzima.

Alipokuwa akitangaza kubadilishwa kwa utaratibu wa kusherehekea Siku ya Uhuru mwaka huu, Rais Magufuli alisema hatua hiyo italiokolea taifa pesa nyingi ambazo hutumiwa katika maandalizi na kufanikisha sherehe hizo.

“Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa sherehe hizo zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka ujao.

Rais John Magufuli aliushangaza umma wa Watanzania pale alipotangaza uamuzi wake wa kufuta sherehe za maadhimisho ya siku y auhuru mwaka huu. Hakungekuwepo na sherehe za matumizi makubwa zinazoambatana na hotuba, muziki na chakula. Badala yake Magufuli alitoa agizo kwa raia kuitumia siku ya Desemba 9 kwa kufanya usafi mitaani na majumbani kwao.

Katika mwezi wa kwanza wa uongozi wake, Magufuli ameendelea kusimama kwa jina laek la utani la "Tingatinga". Akidhamiria kupunguza matumizi yasiyo ya laazima ndani ya serikali, rais huyo wa awamu ya tano, ametangaza kupunguza idadi ya wajumbe watakaoshiriki mkutano wa mwaka wa jumuiya ya Madola nchini Malta kutoka 50 hadi wanne tu.

Na ametangaza huko mbeleni, ni rais, makamu wake na waziri mkuu pekee yao watakaokuwa na haki ya kusafiria madaraja ya juu katika ndege. Maafisa wengine wote wa serikali watasafiria madaraja ya kawaida. Magufuli pia alikata bajeti ya dhifa ya kitaifa ambayo kwa kawaida huambatana na uzinduzi wa bunge. Pesa hizo zilizoookolewa zimetumika kununulia vitanda katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Raia kutoka nchi jirani ya Kenya hasa wanatumia mitandao ya kijamii kueleza namna wangependa kuwa na rais kama Magufuli. "Wakenya wanaamini ni hatua nzuri kwa Tanzania kuwa mfano mzuri. Pengine rais wetu atafuata mfano huo na kupunguza matumizi ya serikali ili Wakenya wame na maisha bora," alisema mwandishi wa habari wa Kenya Fred Ng'etich.

Onyo kwa watumishi wazembe

Magufuli ameapa kupambana na watumishi wazembe serikalini na kutumia fedha za serikali kwa ufanisi zaidi. Amekososa waziwazi vitendo vya rushwa na ubadhirifu ndani ya chama chake tawala CCM, ambacho kimakaa madarakani tangu mwaka 1977. "Natoa ilani kwa watumishi wazembe serikalini kukaa chonjo: Wamevumiliwa kwa muda mrefu, huu ndiyo mwisho wao," alionya katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge.

Hata upinzani unakiri kuwa huu umekuwa mwanzo mzuri kwa rais. lakini kuna hofu kuwa Magufuli anafanya kazi na kuchukuwa maamuzi kivyake bila kuzingatia sheria zilizopo. "Sisi kama bunge, tuna wajibu wa kuunga mkono juhudi zake za kuongeza uwajibikaji nchini, lakini tunapaswa kuhakikisha kuwa haya yote yanfanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni," alisema Zitto Kabwe, moja wa wanasiasa wa upinzani bungeni.

Magufuli ametumia muda mrefu kuliko rais yeyote wa Tanzania kuunda baraza la mawaziri. Chaguo lake la mbunge asiyekuwa maarufu sana Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu, huenda ikawa ishara kuwa kutakuwa na sura mpya zaidi kwenye baraza lake kuchukuwa nafasi za vigogo wa CCM. Wakati wa kampeni zab urais, chama cha CCM kilichagua kaulimbiu ya "Hapa Kazi tu", ikimaanisha awamu hiyo ya tano itakuwa ni ya vitendo zaidi. Miaka mitano ijayo itaonyesha iwapo Magufuli anaweza kudumu na kaulimbiu hiyo.

Mwisho wa habari/ 291