Main Title

source : abna.ir
Jumapili

20 Desemba 2015

20:16:05
726051

Ndege za Israel zavuka mipaka ya Syria na kumuua kiongozi wa Hizbollah + Picha

Mpaka sasa kumeripotiwa kurushwa makombora matatu kutoka Lebanon kwenda Israel, viongozi wa Hizbullah wamesema kuwa makombora hayo hajarushwa na kikosi cha Hibullah na kusisitiza kwamba, Hibullah bado haija anza kujibu kisasi na kisasi chake kitaitetemesha Israel.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ndege za kivita za jeshi la Israel zimevuka mipaka ya Israel na kufanya na kushambulia jengo alilokuwemo kiongozi wa Hizbullah na kumuua.

Ndege hizo za kivita zimemuua Samir Qantwar kiongozi wa Hizbullah katika kitongoji cha Humeh kilichopo mji mkuu wa Syria Damaskas.

Shambulio hilo pia limeuawa watu takriban 10 na wengine wengi kujeruhiwa.

Samir Qantar alishawahi kutumikia kifungo katika gereza za Israel kwa kipindi kirefu, lakini aliachiwa huru katika tukio la kubadilishana mateka baina ya Israel na kundi la Hizbullah baada ya kundi la Hizbullah kushinda vita dhidi ya Israel na  hatimaye Israel kulazimiaka kunyoosha mkono, mnamo mwaka 2006.

Serikali ya Israel ilimuhukumu Samir Qantwar kifungo cha maisha mara tano kwa tuhuma za kuwaua wanajeshi wa Israel watano.

Wananchi wa Israel wameanza kuhama makazi yao kuhifia majibu ya Hizbullah.

Kesho Kiongozi mkuu wa Hizbullah anataraji kuzungumza kwenye vyombo vya habari kutoa msimamo wake kuhusu uchokozi huo wa dhahiri uliofanya na Israel.

Serikali ya Iran imelaani vibaya tukio hilo lililofanywa na Israel na kuliita kuwa ni tukio la kigaidi.

Kiongozi mmoja wa Hizbullah ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa Hizbullah italipa kisasi  kwa nguvu zote.

Mpaka sasa kumeripotiwa kurushwa makombora matatu kutoka Lebanon kwenda Israel, viongozi wa Hizbullah wamesema kuwa makombora hayo hajarushwa na kikosi cha Hibullah na kusisitiza kwamba, Hibullah bado haija anza kujibu kisasi na kisasi chake kitaitetemesha Israel.

Waziri wa Ujenzi wa Israel Yoav Galant kufuatia tukio hilo lilifanywa na nchi yake amesema: Kwa mtazamo wangu watu hatari kama Samir Qantwar ni bora watoweke duniani.

Samiri Qantar alikuwa Syria akiongoza vita dhidi ya magaidi wa Daesh ambao wanaungwa mkono na nchi za Magharibi na Israel.

Kifo cha Samir kimeleta hofu kubwa sana kwa wakazi wa Israel na kujikuta wakisimamisha kazi zao na kuhama makazi yao kwa kuhofia mashambulizi ya kulipa kisasi.

Mwisho wa habari/ 291