Main Title

source : abna.ir
Jumapili

3 Januari 2016

19:35:02
728580

Wananchi wa Qum Iran waandamana kupinga mauji ya Sheikh Nimr yaliyofanywa na serikali ya Saudia arabia

Serikali ya Utawala wa kifalme ya Saudia Arabia imemuua mwanaharakati wanchi hiyo aliyekuwa akitetea haki za wananchi wa nchi hiyo. Sheikh Nimr alikuwa ni mwanazuoni wa dhehebu la Shia na alikuwa akitetea haki za wananchi wa Saudia arabia na kukosoa mienendo miovu ya utawala huo wa kifalme. Kuuawa kwa Sheikh huyu kumezua hisia nzito kwa mataifa mbalimbali Duniani na kusababisha vurugu ndani ya Saudia arabia. Serikali ya Saudia arabia imetangaza kumzika sheikh huyo mahala pa siri bila ya kushirikisha familia ya marehemu.