Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

22 Januari 2016

12:27:40
731490

Picha za Rais wa Tanzania afanya ziara mkoani Arusha akiwa na sale za Jeshi

Dkt Magufuli amekuwa ni rais wa kupigiwa mfano Afrika kutokana na misimamo na misingi yake ya pekee ya Uongozi, jambo lilipelekea rais huyu kupata sifa kila kona ya dunia na kuwa rais wa kupigiwa mfano.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana amewasili Mkoani Arusha ambapo kesho atatunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi wa chuo cha kijeshi wa kundi la 57/15 katika chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli mkoani humo.

Dkt Magufuli amekuwa ni rais wa kupigiwa mfano Afrika kutokana na misimamo na misingi yake ya pekee ya Uongozi, jambo lilipelekea rais huyu kupata sifa kila kona ya dunia na kuwa rais wa kupigiwa mfano.

Rais Magufuli amewasili Mjini Arusha akitokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alikotua kwa ndege akitokea jijini Dar es salaam na kupokelewa na maelfu ya wananchi.

Akiwa uwanjani hapo Rais Magufuli amewashukuru wananchi kwa mapokezi makubwa aliyoyapata na amewaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kazi tu.

"Nawashukuru sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba kuwahakikishia kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu" Alisema Rais Magufuli.

Akiwa njiani kutoka uwanja wa ndege wa KIA, Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa njiapanda ya KIA, Kikatiti, Usa River, Tengeru na Mount Meru Mjini Arusha ambapo huko kote pamoja na kusisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki ni kuchapa kazi, amewahakikishia kuwa hatawaangusha.

"Nataka niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote mpaka yaishe, na naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa mafanikio" Alisisitiza Mheshimiwa Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema tayari serikali imeanza kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu ya Msingi na Sekondari baada ya kufuta ada na akaonya kuwa watumishi wa umma hususani wakuu wa shule watakaothubutu kufanya ubadhilifu wa fedha hizo watashughulikiwa.

Amesema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao na kanda zao na kuwataka watanzania wote kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.

Mwisho wa habari/ 291