Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

22 Januari 2016

19:29:44
731550

Tunisia yatangaza amri ya kutotembea nyakati za usiku kufuatia maandamano + Picha

Serikali ya Tunisia imetangaza amri ya kutotembea nyakati za usiku kufuatia maandamano ya kupinga ukosefu wa ajira nchini humo kusababisha vurugu katika miji kadhaa nchini humo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Tunisia imetangaza amri ya kutotembea nyakati za usiku kufuatia maandamano ya kupinga ukosefu wa ajira nchini humo kusababisha vurugu katika miji kadhaa nchini humo.  Waziri wa mambo ya ndani amesema amri hiyo imewekwa kuanzia saa mbili za usiku hadi saa kumi na moja alfajiri ili kuzuia mashambulizi dhidi ya watu binafisi na mali zao ambayo amesema ni hatari kwa taifa hilo na watu wake. Hapo jana usiku vituo kadhaa vya polisi vilishambuliwa na vyombo vya usalama vikatumia mabomu ya machozi kuwatawanya waaandamaji. Waziri Mkuu Habib Essid alilazimika kukatisha ziara yake nchini Ufaransa na kurejea nyumbani kukabiliana na hali hiyo. Jumapili iliyopita, kijana  mmoja ambaye alipoteza nafasi ya ajira serikalini alipigwa shoti baada ya  kupanda nguzo ya kusafirishia umeme kwa lengo la kuonyesha hisia zake kwa umma kuhusiana na ukosefu wa ajira. Ukosefu wa ajira nchini Tunisia unakisiwa kufikia kiwango cha asilimia 15 kwa ujumla, huku wanaoathirika zaidi na hali hiyo wakiwa vijana.

Mwisho wa habari/ 291