Main Title

source : abna.ir
Jumanne

26 Januari 2016

20:16:29
732152

Shambulizi la Bomu laua Watu 22 Syria + Picha

Takribani watu 22 wameuwawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya kutokea miripuko miwili ya mambomu katika mji unaodhibitiwa na majeshi ya serikali wa Homs.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Takribani watu 22 wameuwawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya kutokea miripuko miwili ya mambomu katika mji unaodhibitiwa na majeshi ya serikali wa Homs.

Gavana wa jimbo la Homs Talal Barazi alisema shambulizi la awali lilikuwa la bomu lililotegwa katika gari na kulenga eneo la kituo cha ukaguzi. Baadae kwa mujibu wa chombo cha habari mhanga aliejifunga mkanda wenye viripuzi alijiripua. Jiji la Homs lilikuwa kiini cha vuguvugu la 2011 la kupinga serikali yanayosababisha machafuko nchini Syria

Kudhibitiwa kwa mji wa Sheikh Maskin

Na katika habari ya faraja kwa upande wa majeshi ya serikali yenye kuungwa mkono na mashambulizi ya anga jeshi la Urusi, na wataalamu wa vita kutoka Iran, yamefanikiwa kuurejesha katika himaya yake mji muhimu uliyopo kusini mwa Syria, baada ya kuwafukuza magaidi wanaoungwa mkono na Saudia arabia na washirika wake, taarifa ambayo imetangazwa vilevile na makundi ya wanaharakati wa haki za binaadamu nchini humo.

Kudhibitiwa kwa Sheikh Maskin, ambao upo kati ya jiji la Damascus na jimbo la kusini la Daraa, kunatokea siku chache baada hatua kubwa ya kusonga mbele kwa majeshi ya serikali katika kaskazini-magharibi na kabla ya mazungumzo ya amani ambayo yamepangwa kufanyika mjini Geneva, yaliyopangwa kufanyika Ijumaa.

Kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria, wanajeshi wa Syria na wanamgambo wa Kilebanon wa Hezbollah wakiongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran waliweza kuweka chini ya himaya yao mji wa Sheikh Maskin baada ya mapigano makali.

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema taifa lake halijamtaka rais Bashar al Assad ajiuzulu na wala kutoa fursa ya hifadhi kwa kiongozi huyo baada ya hatua hiyo, na kusisitiza kwamba Asadi ndiye rais halali wa Syria aliyechaguliwa na wananchi.

Aidha Sergei amgusua suala la maandalizi ya mazungumzo ya amani ya Syria kwa kusisitiza kuwa mazungumzo hayo ya yenye kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa yaliopangwa kuanza wiki hii hayataweza kufanikiwa endapo wawakilishi wa jamii ya Wakurid hawatoalikwa.

Waziri huyo wa Urusi amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP akisema pasipo ushiriki la ujumbe wa kundi hilo la watu hakutakuwa na uwezekano wa kupatikana suluhisho madhubuti la kisiasa nchini Syria- Na kuongeza kwamba jambo hilo lipo katika mamlaka ya mjumbe wa umoja wa matiafa katika mazungumzo hayo Staffan de Mistura,ni kundi la upinzani linalopaswa kualikwa.

Marekani na Uturuki ambazo zinahisa kubwa katika kusababisha vita nchini Syria zinapinga uwepo wa makundi ya kikurdi.

Mwisho wa habari/ 291