Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis leo ameiomba serikali ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kuunga mkono juhudi za amani katika mashariki ya kati, wakati taifa hilo lenye nguvu ambalo ni Jamhuri ya Kiislamu linajitoa kutoka katika hali ya kutengwa kimataifa na kuchukua hatua muhimu kusonga mbele wakati wa ziara ya kwanza ya rais Hassan Rouhani katika makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican.
Baada ya kuondolewa vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa dhidi ya mpango wa amani wa nyuklia ya Iran , rais Rouhani alitumia dakika 40 katika makao makuu ya kanisa Katoliki Vatican kwa mazungumzo ya faragha na papa Francis , muungano mkono mkubwa wa makubaliano na Tehran.
Katika taarifa baadaye, makao makuu ya kanisa hilo yamesema Francis amemuomba kiongozi huyo wa Iran kutumia ushawishi muhimu wa Iran kuhimiza, pamoja na nchi nyingine , suluhisho linalofaa la kisiasa , katika matatizo yanayolikumba eneo la mashariki ya kati na kusaidia kupambana na ugaidi na biashara ya silaha.
Jamhuri ya kiislamu ya Iran ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya kiislamu na ina msaada mkubwa katika kupambana na magaidi wanaodhaminiwa na Saudia arabia mashariki ya kati.
Mwisho wa habari/ 291