Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: majeshi ya utawala halali wa Syria yaumekamata mji muhimu upande wa kusini kutoka mikononi mwa magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na Saudia arabia, wakati muungano mkuu wa upinzani unatarajiwa kujadili iwapo ushiriki katika mazungumzo ya amani mjini Geneva wiki ijayo ama lah .
Kukamatwa kwa mji wa Sheikh Miskeen katika jimbo la kusini la Daraa ni ushindi mkubwa wa hivi karibuni kabisa wa majeshi ya serikali, ambayo yamekuwa yakisonga mbele tangu pale wataalamu wa vita kutoka Iran na majeshi ya Urusi na yalipoanza mashambulizi ya anga nchini humo mwishoni mwa Septemba.
Milio ya mabomu na risasi ilitanda anga la mji huo, huku magaidi wakionekana wakilazimika kukimbia na kiacha asasi na vifaa vyao nyuma huku wengine wengi wakiwa wamekufa na wengine wamejeruhiwa.
Wakati huo huo viongozi wa Umoja wa mataifa wanaohusika na masuala ya kiutu wameziomba pande zinazopigana nchini Syria kuacha kuzishambulia shule, ili kuruhusu wafanyakazi wa kutoa misaada kuwafikia wagonjwa na kuepuka kushindwa kisiasa kumaliza mzozo huo unaoondelea.
Mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Yacoub El Hillo amesema wajumbe watakaoshiriki mazungumzo watambue kwamba sasa inatosha.
Amesema watu milioni 4.5 wanaweza kufikiwa na kupata msaada iwapo mashambulizi ya kijeshi yatakoma.
Mwisho wa habari/ 291