Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

29 Januari 2016

19:35:34
732494

Msikiti wa waislamu wa Kishia wa shambuliwa Saud Arabia + Picha

Shambulio la kigaidi katika msikiti wa waumini wa kiislamu wa dhehebu la shia ambao walikuwa wakitekeleza ibada ya sala ya ijumaa imepelekea kufariki watu wanne na wengine wengi kujeruhiwa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Shambulio la kigaidi katika msikiti wa waumini wa kiislamu wa dhehebu la shia ambao walikuwa wakitekeleza ibada ya sala ya ijumaa imepelekea kufariki watu wanne na wengine wengi kujeruhiwa.

Shambulio hilo lililotokea msikitini wa Imam Kadhim nchini Saud Arabia limesababisha kupoteza maisha ya watu wasiopungua wanne - habari hizo zimetangazwa na kituo kimoja cha televisheni katika nchi hiyo ya kifalme.

Kwa mujibu wa kituo cha Al Arabia,shambulio hilo limetokea katika msikiti mmoja wa mashia katika mkoa wa Iksa wanakoishi watu wengi wa madhehebu ya shia. Mashambulio dhidi ya misikiti ya washia yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara mnamo miezi ya hivi karibuni nchini Saudi Arabia.

Mshambuliaji mwingine ambaye alikuwa akipiga risasi nje ya msikiti huo alikamatwa na waumini na kuawa.

Serikali  ya Saudia arabia ambayo inaongozwa na waislamu wa dhehebu la Answari sunna au wahabia imekuwa ikifanya dhuluma na uadui dhidi ya mashia, ikiwemo kumnyonga mtetezi wa haki za mashia Sheikh Nimr, jambo lililopelekea uhusiano wa Saudia arabia na Iran kuvunjika.

Mwisho wa habari/ 291