Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

5 Februari 2016

16:26:52
733510

NATO yachukizwa na ushindi wa jeshi la Syria dhidi ya magaidi + Picha

Jumuiya ya Kujihami ya NATO imeonyesha kutofurahishwa na ushindi wa jeshi la Syria dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na Saudia arabia na kuungwa mkono na umoja huo.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jumuiya ya Kujihami ya NATO imeonyesha kutofurahishwa na ushindi wa jeshi la Syria dhidi ya magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na Saudia arabia na kuungwa mkono na umoja huo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema kuwa mashambulizi ya angani ya Urusi nchini dhidi ya magaidi nchini Syria "yanahujumu" juhudi za kuutatua mgogoro wa nchi hiyo.

Hayo yamekuja siku chache tu baada ya mashambulizi ya jeshi la serikali ya Syria kuvunj ngome ya magaidi  wanaodhanimiwa na nchi za Ulaya, Marekani na Saudia arabia na kuokoa maelfu ya wananchi waliokuwa wametekwa na kuzuiliwa katika ngome hizo kwa zaidi ya miaka minne, na kusababisha kusitishwa kwa muda mazungumzo ya amani ambayo magaidi hao na walitumia mateka wale kama njia ya kuishinikiza serikali ya Syria.

Akizungumza leo kabla ya kufanya mkutano na mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya, Mkuu huyo wa NATO pia amesema operesheni ya Urusi pia inasababisha ongezeko la mvutano na kuingia katika anga ya Uturuki bila idhini.

Urusi inashutumiwa vikali na nchi za Magharibi kwa kuliunga mkono jeshi la Rais Bashar al-Assad - mshirika mkuu wa Urusi - kwa kufanya mashambulizi ya bomu dhidi ya magaidi wa Daesh tangu mwezi Septemba.

Jeshi la washirika linaloongozwa na Marekani pia linaendeleza madai ya kufanya mashambulizi nchini Syria dhidi ya magaidi wa Daesh lakini ushahidi mwingi umeonyesha kuwa muungano huo unaongozwa na Marekani umekuwa ukiyapa silaha makundi ya kigaidi na hata kuyalinda kwa kuyapa habari za kijasusi.

Muungano wa kijeshi  unaoongozwa na Marekani umekuwa ukishambulia viwanda, visima vya mafuta na miundo mbinu ya Syria  na kudai kuwa inawashambulia magaidi.

Muungano wa wa Urusi, Iran,Syria na Hizbullah umeuthibitishia ulimwengu kwamba magaidi wa Daesh ni kundi dhaifu na linaelekea kuangamia.

Mwisho wa habari/ 291