Main Title

source : abna.ir
Jumatatu

14 Machi 2016

17:29:56
741032

Kundi la kigaidi la waislamu wa dhehebu la Wahabia la Al Qaeda limedai kuhusika na shambulizi lililofanywa katika hoteli tatu zi

Kundi la kigaidi la waislamu wa dhehebu la Wahabia la Al Qaeda limedai kuhusika na shambulizi lililofanywa katika hoteli tatu zilizoko katika mji wa pwani wa Grand -Bassam nchini Cote dìvoire ambapo raia 18 wameuawa

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kundi la kigaidi la waislamu wa dhehebu la Wahabia la Al Qaeda limedai kuhusika na shambulizi lililofanywa katika hoteli tatu zilizoko katika mji wa pwani wa Grand -Bassam nchini  Cote dìvoire  ambapo raia  18 wameuawa . Serikali mjini Abidjan imethibitisha vifo hivyo na kuongeza kuwa wanajeshi wawili nao pia wameuawa katika shambulizi hilo. Duru zinaarifu kuwa miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi hilo ni raia wakigeni kutoka mataiafa ya Burkina Faso, Cameroon, Mali, Ufaransa na Ujerumani. Mji wa Grand Bassam ulioko kilomita 40 kusini mashariki mwa mji mkuu Abidjan ni maarufu kwa raia wa Cote d `voire na wakigeni.

Mwisho wa habari/ 291