Main Title

source : abna.ir
Jumanne

22 Machi 2016

20:52:04
742661

Magaidi wa Daesh wadai kuhusika na shambulizi la Ubelgiji + Picha

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema kile ambacho nchi yake imekuwa inakihofia kimetokea. Waziri Mkuu huyo amewataka wananchi wake wawe watulivu na waonyeshe mshikamamano

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ubelgiji ni moja kati ya nchi za Ulaya ambazo wananchi wake wengi wamejiunga na kikundi cha Kigaidi cha Daesh kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria.

Baadhi ya Magaidi hao wamelazimika kukimbia vita baada ya Majeshi ya Syria kuzidisha mashambulizi dhidi ya magaidi hao na kupelekea magaidi hao kurudi nchini mwao na kuendeleza itikadi za kigaidi walizojipata kutoka katika makundi ya kigaidi na hivyo kulihatarisha bara la Ulaya kwa ujumla.

 Watu zaidi ya 30 wameuawa kutokana na mashambulio ya kigaidi katika mji mkuu wa Ubelgiji-Brussels. Magaidi walifanya mashambulio hayo kwenye uwanja wa ndege na katika kituo cha treni cha chini ya ardhi.

Kwa mujibu wa taarifa watu 14 waliuawa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Brusssels na wengine 20 kwenye kituo cha treni cha chini ya ardhi. Watu wengine zaidi ya 130 walijeruhiwa.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema kile ambacho nchi yake imekuwa inakihofia kimetokea. Waziri Mkuu huyo amewataka wananchi wake wawe watulivu na waonyeshe mshikamamano.

Mashambulio hayo yamewashutusha watu wote barani Ulaya. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere amesema bara lote la Ulaya limelengwa na magaidi waliofanya mauaji hayo.

Ameeleza kuwa sehemu zilizoshambuliwa, uwanja wa ndege na kituo cha treni kilichopo karibu na makao makuu ya Umoja wa Ulaya ni ushuhuda kuwa magaidi hawakuilenga Ubelgiji peke yake bali pia wameyalenga maadili ya Ulaya .

Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema nchi yake imo vitani.

Viongozi wengine kutoka duniani kote pia wameshtushwa na mauaji yaliyotokea mjini Brussels lakini pia wamesisitiza mshikamano na Ubelgiji. Rais Francois Hollande wa Ufaransa ametahadharisha kwamba vita dhidi ya magaidi vitachukua muda mrefu. Hollande ameeleza kuwa magaidi wameishambulia Ubelgiji lakini ni bara la Ulaya lililolengwa.

Viongozi wa wengi wasisitiza mshikamano dhidi ya ugaidi

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls pia amesema kuwa watu wa Ulaya wamo vitani Ameeleza kwamba katika miezi michache iliyopita watu wa Ulaya wamekuwa wanakumbwa na aliyoyaita maafa ya kivita.

Naye Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema mashambulio ya mjini Brusssels kwa mara nyingine yanaonyesha ouvu wa magaidi wanayafuata malengo ya chuki na mauaji.

Katibu Mkuu wa mfungamano wa kijeshi wa NATO Jens Stoltenberg amesema demokrasia haitashindwa lakini amesikitishwa na mauaji ya watu wengi. Amesema "magaidi hawataishinda demokrasia na hatawayaondoa maadili yetu ya uhuru"

Anaewania tiketi ya kukiwakilisha chama cha Demoktratik katika uchaguzi wa Rais nchini Marekani Clinton amesema mashambulio ya magaidi mjini Brussels yataimarisha dhamira ya kusimama pamoja ili kuwashinda magaidi hao na watu wenye itikadi kali.

Kwa mujibu wa taarifa,moja ya shambulio lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Magaidi wa "dola la kiislamu" wamedai kuhusika na mauaji hayo. Baada ya kukamatwa Ijumaa iliyopita, mtuhumiwa mkuu wa mashambulio ya mjini Paris Abdelslam alisema kuwa ameanzisha mtandao mpya na kwamba anapanga mauaji mengine

Hatua za kuimarisha usalama zimechukuliwa barani Ulaya kote.Na nchini Ubelgiji siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa.

Mwisho wa habari/ 291