Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

25 Machi 2016

19:54:00
743154

Vikosi vya Syria vyaukomboa mji wa palmyra + Picha

Wanajeshi wa Syria wameikomboa ngome ya Palmyra toka mikononi mwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wanaosaidiwa na Saudia arabia na Marekani.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wanajeshi wa Syria wameikomboa ngome ya Palmyra toka mikononi mwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wanaosaidiwa na Saudia arabia na Marekani.

Takriban mwaka mmoja baada ya magaidi hao wanadhaminiwa na Marekani na Saudia arabia kuliteka eneo hilo la kale huku ndege za Marekani zikiranda juu na kusababisha magaidi hao kuuchukua mji  huo bila ya kupigwa na ndege za Syria.

Habari hizo zimetangazwa na televisheni ya taifa imliyonukuu duru za kijeshi."Vikosi vyetui vya wanajeshi kwa ushirikiano pamoja na vikosi vya ulinzi vimeikomboa ngome kongwe ya Palmyra na kuwalisha hasara kubwa magaidi wa Daesh" ripoti ya televisheni imesema. Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh wanapewa silaha na Marekani na Saudia arabia na kupa mafunzo ya kijeshi nchini Uturuki na Qatar walizusha wasi wasi na laana kote ulimwenguni walipouteka mji wa Palmyra na ngome kongwe May 23 mwaka jana kwa msaada wa majeshi ya muungano wa Marekani  pamoja na kupandisha bendera yao ya rangi nyeusi na nyeupe huku wakifanya mauaji ya halaiki  ya wananchi wasio na hatia.

Tangu wakati huo magaidi wa Daesh wamekuwa wakivunja mahekalu na kupora mabaki ya kale yanayokadiriwa kujengwa maelfu ya miaka iliyopita pamoja na kumuuwa kiongozi aliyekuwa akisimamia majengo hayo ya kale ya Palmyra, Khaled al-Assaad na kuyauza mabaki hayo kupitia Uturuki, Marekani ni moja kati ya nchi iliyokutwa na mabaki hayo yaliyoibiwa nchini Syria.

Kushindwa kwa magaidi hao katika mji huo kunahesabika kuwa ni pigo kubwa kwa Marekani na washirika wake ambao wamekuwa wakiwasaidia magaidi hao kusonga mbele ili kuiangusha serikali halali ya Syria.

mwisho wa habari/ 291