Main Title

source : abna.ir
Jumatano

30 Machi 2016

17:59:11
744136

Bashar Assad apinga serikali ya mpito inayopendekezwa na washirika wa Saudia arabia + Picha

Marekani na washirika wake baada ya kushindwa kumuondoa rais huyo kwa nguvu za mtutu sasa wanajitahidi kutaka kumtoa kwa uongo wa siasa jambo ambalo halikubaliki kabisa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema nchi hiyo inahitaji serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itaongoza mchakato wa kupatikana katiba mpya, na akapinga "serikali ya mpito" inayodaiwa na upinzani unaounga mkono na Saudia arabia na nchi za magharibi ambao unamtaka ajiuzulu. Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Urusi, Assad amesema wakimbizi wa Kisyria wataanza kurejea nyumbani wakati watakapoona matumaini ya maendeleo, akiongeza kuwa mojawapo ya sababu kuu za uhamiaji ni vikwazo vya kidhalimu vilivyowekwa na nchi za magharibi dhidi ya Syria.

Dk: Assad amesema maneno ya "mpito wa kisiasa" yana maana kuwa mabadiliko kutoka kwa katiba moja hadi nyingine na hivyo kipindi cha mpito lazima kiwe chini ya katiba ya sasa, na watahamia katika katiba mpya ikiwa watu wa Syria wataipigia kura.

Marekani na washirika wake baada ya kushindwa kumuondoa rais huyo kwa nguvu za mtutu sasa wanajitahidi kutaka kumtoa kwa uongo wa siasa jambo ambalo halikubaliki kabisa.

Mwisho wa habari/ 291