Main Title

source : abna.ir
Jumatano

30 Machi 2016

18:20:22
744144

Amiri jeshi mkuu wa Iran: Iran inahitaji nguvu za makombora zaidi + Picha

Amiri jeshi mkuu wa Iran Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesisitiza jeshi lake kuwa linatakiwa kujiimarisha zaidi katika kila sekta hasa sekta ya makombora.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Amiri jeshi mkuu wa Iran Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesisitiza jeshi lake kuwa linatakiwa kujiimarisha zaidi katika kila sekta hasa sekta ya makombora.

Amiri jeshi mkuu huyo ameyasema hayo leo katika hafla ya kuazimisha siku ya wanawake duniani

Ambapo kwa waislamu wa dhehebu la Shia huadhimisha siku hiyo kufuata kuzaliwa kwa Bi Fatma bint wa mtume Muhamad s.a.w.

Amiri jeshi mkuu huyo ameendeleza kusema kuwa Iran inatakiwa iwe na uchumi wa hali ya juu pia iwe na nguvu za kijeshi za kutosha kiasi ambacho adui aihofu Jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Kiongozi huyo ameyasema hayo kufuatia Marekani na washirika wake kuandika barua kwa baraza la uslama la Umoja wa mataifa na kuomba Iran iwekewe vikwazo kutoka na kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, ambayo kwa mujibu wa Marekani na washirika wake, Makombora hayo yanauwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia.

Siku ya leo ambayo ni siku maalamu ya kuadhimisha hadhi na heshima ya mwanamke katika uislamu, waislamu wa dhehebu la Shia wanaitumia siku hii kutoa zawadi maalumu kwa wanawake hasa wazazi ndugu na wake zao.

Dhehebu la shia ni dhehebu la kiislamu linalomfuata mtume Muhammad s.a.w na kizazi chake pekee kama viongozi wa Umma wa kiislamu, tofauti na madhehebu mengine ambayo yanamfuata mtume na maswahaba.

Mwisho wa habari/ 291