Main Title

source : abna.ir
Jumatano

6 Aprili 2016

18:18:49
745646

Gaidi mla maini ya watu auawa Syria+ Picha

Abu Siqaar Mpiganaji maarufu wa kundi la kigaidi la Daesh linalodhaminiwa na Saudia arabia, ambaye alitikisa ulimwengu kwa kumuua kumtoa maini mwanajeshi wa Syria akiwa hai na kuyatafuna maini hayo, huku akijigamba kuwa wataendelea kuwaua waislamu wa madhehebu ya Shia wote na kusimamisha dola la kiislamu la kisuni.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Abu Siqaar Mpiganaji maarufu wa kundi la kigaidi la Daesh linalodhaminiwa na Saudia arabia, ambaye alitikisa ulimwengu kwa kumuua kumtoa maini mwanajeshi wa Syria akiwa hai na kuyatafuna maini hayo, huku akijigamba kuwa watawaua waislamu wa madhehebu ya Shia wote na kusimamisha dola la kiislamu la kisuni.

Jina halisi la Gaidi huyu ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha kigaidi cha Omar al faruk , ni Khalid Ahmad ambapo lakabu yake ni Abu Siqaar, Gaidi huyu aliuawa na majeshi ya Syria katika mji wa Latikia.

Kitendo hicho kilitoa picha halisi ya magaidi hao wa Daesh ambao ni waislamu wa dhehebu la Sunni wahabia au maarufu kama waislamu wa Siasa kali , wanaodhaminiwa na Saudia arabia.

Magaidi wa Daesh wamekuwa wakibaka wanawake na watoto, wamekuwa wakichinja na kuua watu kinyama na pia wamekuwa wakiiba mali na kuuza wanawake katika nchi za kiarabu na Israel haya yote wanayafanya wakijinadi kuwa wanawakilisha uislamu.

Serikali ya Iran ilituma wataalamu wake wa vita kuzisaidia serikali za Syria na Iraq kupambana na magaidi hao hatari, lakini Saudia arabia ikishirikiana na Marekani na Uturuki walitengeneza Muungano wa nchi 61 wakidai kupambana na kundi hilo lakini ukweli ukafichuka kwamba nchi hizo zinalipatia kundi hilo silaha na mafunzo ya kijeshi ili kuziangusha serikali za Syria na Iraq.

Saudia arabia na nchi za kiarabu zinazojinadi kuwa ni nchi za kisuni zimekuwa zikiwasaidia magiadi hao kwa lengo la kupambana na serikali za Syria na Iraq ambazo ni serikali za kishia hivyo nchizi zilitumika kuwashawishi waislamu wa dhehebu la Suni kwenda kujiunga na makundi hayo kwa madai ya jihadi, ambapo wapiganaji jihadi wa makundi hayo ya kigaidi hupewa wanawake na pesa nyingi ambazo vyombo vya kijasusi vinasema kuwa mpiganaji mwenye ustadi wa kijeshi analipwa dola 700 kila siku.

Uturuki imekuwa ikilitumia kundi hilo kuwaua wapiganaji wa kikurdi ambao wanasadikiwa kuwa dhidi ya serikali ya Uturuki.

Na Marekani imekuwa ikiwatumia magaidi hao kuziangusha serikali za Syria na Iraq ili iweze kurudisha majeshi yake na kutawala sehemu hizo kwa madai ya kupambana na magaidi.

Lakini nyama hizi potovu za Marekani , Saudia arabia na washirika wao zimeishia patupu baada ya serikali ya Iran kumtuma Jeneral Qassim Suleiman mtaalamu wa vita kutoka Iran, ambapo amevunja njama hizo zote.

 

 

 

Mwisho wa habari/ 291