Main Title

source : abna.ir
Jumatano

13 Aprili 2016

14:47:02
747067

Uchaguzi waendelea Syria wakati mazungumzo ya amani yakiaanza tena leo + Picha

Duru mpya ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza vita nchini Syria vinavyochochewa na Marekani, Saudia arabia, Uturuki na washirika wao vilivyodumu miaka mitano sasa yameanza leo jijini Geneva.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Duru mpya ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza vita nchini Syria vinavyochochewa na Marekani, Saudia arabia, Uturuki na washirika wao vilivyodumu miaka mitano sasa yameanza leo jijini Geneva.

Hayo yanajiri wakati mapigano makali yakiendelea kati ya wanajeshi wa Syria na makundi ya waasi na magaidi wanaodhaminiwa na Marekani na washirika wake katika mkoa wa kaskazini Aleppo ambao wamekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa yanalenga kuunda serikali ya mpito nchini Syria itakayofuatwa an uchaguzi mkuu wa kumaliza mzozo huo unaochochewa na nchi za kigeni ambao umewauwa zaidi ya watu 270,000 na kuiacha nusu ya idadi ya watu nchini humo bila makazi.

Hatima ya Rais Bashar al-Assad inasalia kuwa kizuizi katika mazungumzo hayo, na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amefanya mikutano na washirika wakuu wa Assad ambao ni Iran na Urusi kabla ya kukutana leo na Kamati Kuu ya Mazungumzo inayouwakilisha upinzani, na kisha wawakilishi wa serikali baadaye wiki hii.

Kuongezeka kwa machafuko katika siku chache zilizopita kumetishia mpango wa kihistoria wa kusitisha mapigano uliosainiwa mwezi Februari ambao unaendelea kuheshimiwa kwa kiwango kikubwa  na kuongeza shinikizo kwa mazungumzo haya, ambayo yanafuata majaribio mawili ya awali yaliyoshindikana ya kutafuta ufumbuzi wa kumaliza muwagaji damu nchini humo ambapo magaidi wanaopewa mafunzo na Marekani na kudhaminiwa na nchi za kiarabu wameendelea kuua watu hovyo ili kutimiza malengo ya Marekani, Umoja wa Ulaya na washirika wao ya kutaka kuangusha serikali halali ya Syria.

Suala jingine la mvutano wakati mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja yakianza ni uchaguzi wa bunge unaoandaliwa leo katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali kote nchini humo. Umoja wa Mataifa umedai kuwa hauutambui uchaguzi huo, ambao pia umepuuzwa na wapinzani wa Assad ndani na nje ya Syria wakisema sio wa haki.

Rais Bashar al Assad na mkewe Asma wamepiga kura zao mjini Damascus. Uchaguzi wa bunge nchini Syria huandaliwa kila baada ya miaka minne, na serikali inasema uchaguzi huo ni wa kikatiba na uko tofauti na mazungumzo ya amani yanayoendelea Geneva.

Mpango huo wa kuwekwa chini silaha umewezesha kupelekwa misaada ya kiutu katika maeneo yaliyoathirika na pia kupungua kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya raia. Bettina Lüscher ni Msemaji wa Mpango wa Chakula Duniani - WFP "Hii itachukua wiki kadhaa, na tutaendeleza juhudi hizi, na kujaribu kuwasiliana na watu walioko katika maeneo yaliyoathirka kuona namna tunavyoweza kuyafikia. Lakini tunaendeleza operesheni hadi tutakapowafikia watu wote wanaohitaji chakula. Lakini bila shaka kwa kufanya hesabu, itachukua muda mrefu".

Wakati huo huo majeshi yanayoiunga mkono serikali halali ya Syria yameendelea kusonga mbele katika mji wa Al-Eis unaodhibitiwa na kundi la kigaidi la An nusra linalidhaminiwa na Marekani na Saudia arabia lenye mafungamano na al-Qaeda, na waasi washirika. Shirika linalofchunguza haki za binaadamu nchini Syria limesema kundi la Al-Nusra na na makundi mengine ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani walipigana na vikosi hivyo na kuwawau wanajeshi 23 watiifu kwa Assad, wakiwemo wapiganaji wa Kiiran na Kiafghanistan, huku mamia ya wapiganaji wa kundi hilo waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Wapiganaji kama hao kutoka kundi la kigaidi la al-Nusra Front na kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu wanaodhaminiwa na Marekani hawashirikishwi katika mpango wa kusitisha mashambulizi. Lakini katika baadhi ya maeneo, makundi ya kigaidi la Daesh na al-Nusra yanashirikiana na wapiganaji wa waasi wanaostahili kushirikishwa na mpango huo hivyo inakuwa ni vigumu kwa jeshi la Syria kuchagua nani wa kuua na nani wa kuacha.

Mwisho wa habari/ 291