Main Title

source : abna.ir
Jumamosi

14 Mei 2016

11:26:04
754121

Israel yamuua Kamanda wa kundi la Hezbollah + Picha za Mazishi

Kikundi Harakatu Nujabaa ambacho maalum cha makomando kinachukusanya wapiganaji wenye uwezo wa hali ya juu ambao wanapambana na magaidi nchini Syria , kimetoa tanzia zake kufuatia kifo cha kamanda huyo na kuahidi kwamba: Israel imejifungulia milango ya moto, hivyo isubiri moto wa mashambulizi mazito ya kisasi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la Hezbollah ameuliwa nchini Syria, kufuatia shambulizi lilofanywa karibu na uwanja wa ndege wa mjini Damascus.

Kamanda huyo mkuu ameuawa bomu lililorushwa na ndege za jeshi la Israel huko Syria.

Mustafa Badreddine alikuwa ni moja kati ya makamanda wa Hizbullah wanaoongoza vikosi vya jeshi vinavyoiunga mkono serikali ya Syria katika kupambana na magaidi nchini Syria wakiwemo wale magaidi wanaodhaminiwa na Saudia arabia, Marekani na washirika wao.

Taarifa ya viongozi wa kundi hilo la kijeshi na kisiasa la waislamu wa dhehebu la Shia, imesema uchunguzi bado unaendelea .

Badreddine alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Hezbollah walioongoza vita vya siku 33 baada ya majeshi ya Israel kuivamia Hizbullah.

Katika vita hivyo kundi la Hizbullah ambalo linadhaminiwa na kupewa mafunzo ya kijeshi na Iran lilifanikiwa kulishinda jeshi la Israel na kulifanya jeshi la Israel kunyenyua mikono juu na kukili kushindwa vita.

Baada ya vita hivyo vilivyoipatia serikali ya Israel hasara kubwa, serikali ya Israel imekuwa ikiwawinda viongozi wa  kundi la Hizbullah na kuwaua.

Jenerali Vahidi ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wa Iran, amesema : majeshi ya Iran yatalipa kisasi kwa Israel muda muafaka utakapofika.

Licha ya kuwa baadhi ya viongozi wa Israel wanaasili ya Iran, pande hizi mbili zinauadui mkubwa sana.

Iran ambayo ni taifa la kiislamu linapinga kabisa taifa la kidhalimu la Israel ambalo limepatikana kwa kuporwa ardhi wananchi wa Palestin, Lebanon na Syria.

Serikali ya Iran inasisitiza kwamba utawala dhalimu wa Israel unatakiwa kuangamizwa na utaangamizwa muda muafaka ukifika.

Serikali ya Israel ni moja kati ya nchi zinazoongoza kwa mauji ya kiholela, kuvuka mipaka ya nchi nyingine na kukiuka haki za binadamu lakini Umoja wa mataifa unakalia kimya jinai za nchi hiyo inayoungwa mkono na mataifa makubwa ikiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa na washirika wao.

Kikundi Harakatu Nujabaa ambacho maalum cha makomando kinachukusanya wapiganaji wenye uwezo wa hali ya juu ambao wanapambana na magaidi nchini Syria , kimetoa tanzia zake kufuatia kifo cha kamanda huyo na kuahidi kwamba: Israel imejifungulia milango ya moto, hivyo isubiri moto mkali wa mashambulizi mazito ya kisasi.

Mwisho wa habari/ 291