source : abna.ir
Jumamosi
2 Julai 2016
15:31:20
763692
Picha za wananchi wa Thailand wakiandamana kupinga dhulma dhidi ya Palestina katika siku ya Quds
Siku ya Quds ni siku ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Siku hii iliasisiwa na kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran Ayatollah Khomeini kwa ajili ya kutetea haki za wananchi wa Palestina wanaodhulumiwa na Israel inayosaidiwa na mataifa makubwa ikiwemo Uingereza na Marekani na hata baadhi ya mataifa ya kiarabu pia yamekuwa yakishiriki katika kuwakandamiza wapalestina. Siku hii ambayo imeanzishwa na kiongozi wa dhehebu la Shia la kiislamu imepokewa vizuri na madhehebu mengine ya kiislamu na hata dini nyingine.