Main Title

source : abna.ir
Jumamosi

15 Oktoba 2016

19:25:24
785736

Bomu laua watu zaidi ya 35 kaskazini mwa Baghdad + Picha

Shambulio la bomu lililofanywa na magidi lililowalenga waislamu wa dhehebu la Shia ambao walikuwa katika maombolezi ya kifo cha Husein mjukuu wa Mtume Muhammad kaskazini mwa Baghdad Iraq,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Shambulio la bomu lililofanywa na magidi lililowalenga waislamu wa dhehebu la Shia ambao walikuwa katika maombolezi ya kifo cha Husein mjukuu wa  Mtume Muhammad kaskazini mwa Baghdad Iraq, limewaua watu  zaidi ya 35 na kuwajeruhi wengine 63. Maafisa wa polisi na wale wa hospitali wamethibitisha idadi hiyo na hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, ambalo limekuja wakati vikosi vya Iraq vikijiandaa kwa ajili ya operesheni ya kuukomboa mji wa Mosul ulio wa pili kwa ukubwa nchini Iraq unaoshikiliwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh. Katika siku za nyuma kundi hilo la kigaidi lenye kusadikiwa kuwa na uhusiano na Uturuki na Marekani limeongeza mashambulizi katika maeneo ya ndani yanayodhibitiwa na serikali mbali kabisa na maeneo yalioko mstari wa mbele wa mapambano hiyo ikiwa ni baada ya kupoteza udhibiti katika uwanja wa mapambano wenyewe. Iraq imekuwa ikishuhudia mashambulizi ya mabomu katika miezi ya hivi karibuni.

Magaidi wa Daesh hapo awali walikuwa wakishambulia na kuteka miji na kufanya ufisadi mkubwa lakini baada ya Iran kutuma wataalamu wake wa vita kwa ajili ya kuzisaidia serikali za Syria na Iraq, magaidi wa kundi hilo wamekuwa wakirudishwa nyuma, huku wengi wakiuawa na wengine wakilazimika kuyakimbia maeneo waliyoyateka .

Mwisho wa habari/ 291