Main Title

source : abna.ir
Jumatatu

21 Novemba 2016

20:48:54
793421

Kundi la kigaidi la Daesh laua watu 30 msikitini Afghanistan + Picha

Kundi la kigaidi Daesh linalojulikana kwa jina la Dola la Kiislamu, IS, limekiri kuhusika na mauaji ya waislamu waliokuwa katika ibada ya sala ya adhuhuri katika mji wa Kabul Afghanistan.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kundi la kigaidi Daesh linalojulikana kwa jina la Dola la Kiislamu, IS, limekiri kuhusika na mauaji ya waislamu waliokuwa katika ibada ya sala ya adhuhuri katika mji wa Kabul Afghanistan.

Kundi hilo la kigaidi linalosadikiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Saudia arabia na Uturuki limekiri kufanya mashamulizi dhidi ya msikiti mmoja wa waislamu wa dhehebe wa shia waliokuwa katika ibada katika mji mkuu wa Afghanistan, ambapo watu 30 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa vibaya. Taarifa ya kundi hilo kupitia shirika la habari la Aamaq, inasema kuwa mshambuliaji wao wa kujitoa muhanga ndiye aliyejiripua katika msikiti huo uliokuwa umejaa watu, magharibi mwa Kabul. Msemaji wa wizara ya afya, Mohammad Ismail Kawusi, amesema watu wengine 85 ikiwa ni pamoja na watoto na kiasi cha wanawake saba ni miongoni mwa waliojeruhiwa. Mkuu wa idara ya uchunguzi wa jinai, Faraidon Obaidi, alitoa hapo kabla idadi ya watu waliouwawa kuwa 27 na kusema watu wengine 35 wamejeruhiwa.Waumini wa dhehebu la Shia walikusanyika katika msikiti huo kuadhimisha siku ya arobaini ya kifo cha Hussein  mjukuu wa mtume Muhammad, ambaye aliuliwa kwa kukatwa kichwa na maswahaba waovu wa mtume Muhammad katika mji wa Karbalaa Iraq. Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan ameyalaani mashambulizi hayo dhidi ya waumini katika msikiti, akisema ni tukio lisiliosahaulika na uhalifu mkubwa. Mtendaji mkuu wa Afghanistan, Abdullah Abdullah, ameyaita mashambulizi hayo kuwa ni uhalifu wa kivita.

Mwisho wa habari/ 291