Main Title

source : Pars Today
Jumamosi

15 Juni 2019

07:52:47
951084

Maulama wa Palestina: Kikao cha Bahrain kina lengo la kuifuta Palestina na kusambaratisha matukufu ya Wapalestina

Jumatano yana Jumuiya ya maulama wa Palestina ilifanya kikao kilichopewa jina la 'Maulama wa Palestina katika Kukabiliana na Mpango wa Muamala wa Karne wa Trump' huko Ukanda wa Gaza kwa lengo la kujadili malengo ya mkutano wa kiuchumi wa nchini Bahrain.

(ABNA24.com) Jumatano yana Jumuiya ya maulama wa Palestina ilifanya kikao kilichopewa jina la 'Maulama wa Palestina katika Kukabiliana na Mpango wa Muamala wa Karne wa Trump' huko Ukanda wa Gaza kwa lengo la kujadili malengo ya mkutano wa kiuchumi wa nchini Bahrain.

Katika kikao hicho maulama hao walisema lengo la mkutano huo wa Bahrain ni kufuta kadhia ya Palestina na kusambaratisha matukufuu ya Wapalestina. Aidha mwishoni mwa mkutano huo, Marwan Abu Raas, Mkuu wa Jumuiya ya Maulama wa Palestina alisoma taarifa ya kikao hicho ambapo alitoa mwito kwa raia wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kuunga mkono muqawama na kuwatetea wananchi wa Palestina. Alisema kuwa Muamala wa Karne ni jinai ya kisiasa dhidi ya Uislamu, raia na wanaadamu ambao licha ya kutekelezwa kwa kisingizio cha kustawisha uchumi, lakini lengo lake hasa ni kukiuka wazi haki za Wapalestina na kufuta kadhia ya Palestina.

Kadhalika akiashiria kufungamana Wapalestina na haki ya kurejea kwenye ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Marwan Abu Raas amezitaka pande zote za Palestina kuweka kando tofauti zao na kuelekea kwenye njia ya umoja wa kitaifa. Mkutano wa kiuchumi wa Manama, mji mkuu wa Bahrain ulioitishwa na Marekani umepangwa kufanyika tarehe 25 na 26 za mwezi huu ambapo katika jukwaa hilo kutatangazwa kuvutia uwekezaji zaidi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kwa madai eti ya kuboresha hali ya kiuchumi ya Wapalestina. Mpango wa Muamala wa Karne ambao unadaiwa na Wamarekani kuwa utahitimisha mzozo wa Wapalestina na Wazayuni, mbali na kufuta kabisa ndoto ya kurejea makwao wakimbizi wa Kipalestina, unawazuia pia kuunda nchi yao huru sambamba na kubariki rasmi uvamizi wa utawala wa Kizayuni na kuufanya uendelee kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.



/129