Main Title

source : Pars Today
Jumatano

19 Juni 2019

09:42:47
952685

Meja Jenerali Bagheri: Mafuta ya nchi nyingine hayatauzwa nje kwa amani mpaka ya Iran yauzwe

"Iwapo Iran itataka kuzuia uuzaji nje wa mafuta ya Ghuba ya Uajemi itatangaza suala hilo waiwazi na haitaficha suala hilo na kufanya hadaa kama inavyofanya Marekani na vibaraka wake wa kikanda na kimataifa."

(ABNA24.com) "Iwapo Iran itataka kuzuia uuzaji nje wa mafuta ya Ghuba ya Uajemi itatangaza suala hilo waiwazi na haitaficha suala hilo na kufanya hadaa kama inavyofanya Marekani na vibaraka wake wa kikanda na kimataifa."

Haya yamesemwa na Kamanda wa Majeshi ya Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri katika mazungumzo yake na waandishi wa habari mjini Tehran. Ameashiria hadaa na uongo unaoenezwa na Marekani kuhusu mlipuko uliotokea katika bandari ya Fujairah huko Imarati na milipuko iliyotokea katika meli mbili za mafuta katika Bahari ya Oman na kusema: Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linafuatilia harakati zote za maadui kwa umakini mkubwa. 

Alkhamisi iliyopita vyombo vya habari viliripoti habari ya kutokea milipuko katika meli mbili za kubeba mafuta kwenye Bahari ya Oman. Baada tu ya kuripotiwa habari hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo aliituhumu Iran kuwa ndiyo iliyohusika na milipuko hiyo bila hata ya kutoa ushahidi wowote wa kuthibitisha madai yake. Muda mfupi baadaye Mshauri wa Masuala ya Nje wa Saudi Arabia, Adel al Jubeir alijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kukariri madai yasiyo na msingi ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. 

Hii si mara ya kwanza kwa eneo la Ghuba ya Uajemi kushuhudia matukio kama haya. Migogoro inayosababishwa na uingiliaji kati wa madola ya kigeni inatokana na siasa na sera za kibeberu na za kutaka kujitanua zaidi za madola makubwa. Historia inaonesha kuwa, badala ya kufanya jitihada za kuimarisha amani na usalama katika eneo hilo, madola hayo huwa kizuizi na pingamizi kubwa zaidi la amani katika kanda ya Ghuba ya Uajemi. 

Inatupasa kusema hapa kuwa, kwa kukariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran, Mshauri wa Masuala ya Nje wa Saudi Arabia, Adel al Jubeir ameonesha jinsi alivyo mwanagenzi au anavyotaka kujifanya kwamba hajui historia ya eneo la Ghuba ya Uajemi. Miaka mingi iliyopita Marekani ilianza kutekeleza kifungu cha nne cha mpango wa Truman uliopewa jina la "Point Four Program" kwa ajili ya malengo makuu mawili ambayo kwanza ni kuzuia kupanuka na kupata ushawishi zaidi ukomunisti, na pili kutumia utajiri wa mafuta na nafasi ya kistratijia ya nchi za Ghuba ya Uajemi kwa ajili ya kutumikia siasa za Marekani.

Japokuwa mpango huo wa Point Four Program wa aliyekuwa rais wa Marekani, Harry S. Truman ulitumiwa katika propaganda za utawala wa nchi hiyo kwa kisingizio cha kuzisaidia nchi maskini, lakini kwa hakika ulikuwa mwavuli unaotumiwa na serikali ya Washington kuwahadaa walimwengu kwa ajili ya kudhibiti na kupora utajiri na maliasili za nchi maskini na zilizobakia nyuma. Sera hiyo inaonekana waziwazi katika fikra na utendaji wa Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump ambaye ameitaja Saudi Arabia kuwa "gombe lenye maziwa" ambalo linapaswa kukamuliwa.

Wakati huo huo, licha ya kwamba Saudi Arabia ni sehemu ya siasa na nyenzo za Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, laiki inaonekana kuwa inafanya jitihada za kuanzisha mlingano ambao upande wake mmoja ni kuvuruga amani na usalama wa Iran. Hata hivyo upande wa pili wa mlingano huo unaionekana kuwa kizungumkuti kwa Saudia na hata kwa Marekani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, Iran haifuati siasa na maamuzi ya Marekani na Riyadh.

Baadhi ya nchi zenye watawala vibaraka zinadhani kuwa zinaweza kulinda uwepo wa tawala zao kupitia njia ya kuzusha migogoro na kuyyakaribisha majeshi ya kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Hata hivyo inapaswa kuwa wazi kwamba, hii ni njozi na dhana potofu. Utawala wa Riyadh unafuata kibubusa na kutekeleza mradi wa Marekani na Israel wa kutaka kuidhihirisha Iran kuwa ni tishio. Hata hivyo ukweli ni kwamba, Saudi Arabia imenasa katika mtego wa kistratijia wa Marekani na Israel. Haya ni makosa ya kistratijia yanayowakumba pia watawala wa Imarati na hatima yake ni kugonga mwamba.

Mwandishi na mchambuzi mashuhuri wa Marekani, Jim W. Dean anasema: "Nchi za (Kiarabu) za Ghuba ya Uajemi zimekuwa wawakilishi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na kambi za kijeshi za kuzidisha uwezo wa Marekani katika eneo hilo."

Mwishoni mwa uchambuzi huu inatupasa kuashiria matamshi ya Mkuu wa Majeshi ya Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri ambaye amesema: Iran ni mlinzi wa lango bahari la Hormuz na Ghuba ya Uajemi na inautambua usalama na amani ya eneo hilo kuwa ni sawa na usalama wake.

Meja Jenerali Bagheri ameongeza kuwa, Iran itaendelea kulinda usalama wa eneo hilo maadamu hawajaanzisha matatizo, lakini amesisitiza kuwa: Mafuta ya nchi nyingine hayatauzwa nje kwa amani hadi pale mafuta ya Iran yatakapouzwa katika masoko ya kigeni. 




/129