Main Title

source : Pars Today
Jumamosi

22 Juni 2019

06:28:39
953483

Matokeo hasi ya kiuchumi ya siasa za vita za watawala wa Saudia

Taathira hasi zinazotokana na siasa za kupenda vita za watawala wa Saudi Arabia zimeanza kuonekana wazi katika soko la hisa la nchi hiyo ya kifalme.

(ABNA24.com) Taathira hasi zinazotokana na siasa za kupenda vita za watawala wa Saudi Arabia zimeanza kuonekana wazi katika soko la hisa la nchi hiyo ya kifalme.

Kuwepo mfungamano wa moja kwa moja kati ya uchumi na amani ni jambo la kawaida kabisa. Ghasia na machafuko huathiri pakubwa uchumi kama ambavyo usalama na amani pia husaidia pakubwa kustawisha uchumi wa nchi yoyote ile na kuvutia wawekezaji wa kigeni. ukweli huo unaoonekana wazi katika baadhi ya maeneo ya dunia na hasa eneo la Asia Magharibi ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta.

Katika miaka michache iliyopita harakati za makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudia katika nchi za Iraq na Syria pamoja na vita vya kichokozi vya utawala wa Riyadh  kilihesabiwa kuwa chonza muhimu cha kuvurugika usalama wa Asia Magharibi lakini hivi sasa Saudia ndio sababu kuu ya kuvurugika usalama wa eneo hili muhimu. Kudumishwa mashambulio ya kinyama nchini Yemen, udiplomasia wa kuibua ghasia na kuichochea Marekani iishambulie kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni siasa za vita zinazofuatiliwa kwa karibu na watawala wa Riyadh katika eneo hili la Asia Magharibi. Siasa hizo sambamba na kuongezeka uwezo wa kiulinzi na kihujuma wa wapiganaji wa Yemen ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakishambulia vituo muhimu vya mafuta vya Saudia, kumepelekea uchumi wa nchi hiyo kuathirika pakubwa kutokana na siasa za kupenda vita za watawala wa nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo nchi kama Qatar ambayo  katika miaka ya karibuni imeamua kutupilia mbali siasa kama hizo za kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine na kuchagua siasa za kuimarisha amani na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati imeshuhudia uchumi wake ukistawi na kuimarika katika nyanja mbalimbali.

Matokeo mabaya ya siasa za kupenda vita za watawala wa Saudia hayaonekani tu katika soko la hisa la nchi hiyo bali hata kwenye sera za kiuchumi za nchi hiyo. Katika ripoti yake iliyotolewa mwezi uliopita, Shirika la Kimatifa la Fedha IMF limetabiri kwamba Saudia mwaka ujao itakumbwa na nakisi kubwa ya bajeti ya asilimia 7.2 hata tukifaradhisha kuwa nchi hiyo itaendelea kuuza nje mapipa milioni 10.2 ya mafuta kwa siku ambapo kila pipa litakuwa likiuzwa kwa dola 65.5. Shirika hilo la kimataifa linaloshughulikia masuala ya fedha limetabiri kuwa uchumi wa nchi hiyo mwaka huu utakuwa kwa asilimia 1.9 pekee, ambapo iwapo hilo litathibiti kiwango cha ukuaji wa uchumi huo kitakuwa kimepungua kwa asilimia .3 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Hilo pia ni kwa kutegemea bei ya mafuta ya dola 65 kwa  pipa. Hii ina maana kuwa iwapo bei hiyo itapungua na kila pipa la mafuta kuuzwa kwa bei iliyo chini ya dola 65, uchumi wa nchi hiyo utapata pigo kubwa zaidi.

Nukta ya mwisho na ya kusikitisha ni kwamba, licha ya kudhihirika wazi matokeo mabaya ya siasa za kupenda vita za watawala wa Aal Saud kwa uchumi wa nchi hiyo, lakini bado wamefumbia macho ukweli huo na kuendelea kufuatilia siasa hizo mbovu za kuchochea machafuko na ghasia katika eneo hili tata la Asia Magharibi.



/129