Main Title

source : Pars Today
Jumatano

26 Juni 2019

08:23:29
955211

Iran ni miongoni mwa nchi zinazoshirikiana zaidi kimataifa kuhusu suala la haki za binadamu

Licha ya kuwa suala la haki za binadamu kidhahiri lina wafausi na watetezi wengi lakini ukweli wa mambo ni kuwa suala hilo linatumiwa na watetezi hao wa kidhahiri kwa shabaha ya kufikia malengo yao ya kisiasa.

(ABNA24.com) Licha ya kuwa suala la haki za binadamu kidhahiri lina wafausi na watetezi wengi lakini ukweli wa mambo ni kuwa suala hilo linatumiwa na watetezi hao wa kidhahiri kwa shabaha ya kufikia malengo yao ya kisiasa.

Kuna undumakuwili mkubwa unaotekelezwa katika ngazi za kimataifa kuhusiana na suala la haki za binadamu, na hata katika nchi zinazodai kuwa mstari wa mbele wa kutetea haki hizo zikiongozwa na Marekani, Canada na Ufaransa. Madamu undumakuwili huo utaendelea kuwepo ni wazi kuwa suala la haki za binadamu nalo litaendelea kuwa muhanga wa tamaa za kisiasa na maslahi haramu ya kifedha katika upeo wa kimataifa.

Akiashiria suala hilo siku ya Jumatatu katika kikao na mabalozi, manaibu balozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa hapa mjini Tehran, Sayyid Ibrahim Raisi, Mkuu wa Vyombo vya Mahakama hapa nchini alikosoa vikali undumakuwili unaoonyeshwa na nchi za Magharibi kuhusiana na suala zima la haki za binadamu. Raisi ametoa mifano kadhaa inayothibitisha wazi undumakuli huo wa nchi za Magharibi kuhusiana na suala la haki za binadamu.

Kimya cha taasisi na mashirika ya kimataifa kuhusiana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina, kuendelea jinai za Saudia Arabia zinazotekelezwa kwa ushirikiano wa moja kwa moja wa Marekani na washirika wake na ambazo zimesababisha wahanga zaidi ya 60,000 na kukosolewa hatua za baadhi ya nchi zinazojiepusha kutuma nchini Iran dawa na zana za tiba kwa kisingizio cha kuwepo vikwazo vya Marekani, ni sehemu muhimu ya hutuba iliyotolewa na mkuu huyo wa vyombo vya mahakama vya Iran katika kikao cha Jumatatu mjini Tehran.

 Marekani na nchi za Ulaya zinazungumzia suala la haki za binadamu katika hali ambayo zinavunja wazi wazi haki za msingi kabisa za binadamun hata kwenye jamii zao zenyewe. Robert Fantina mtafiti wa masuala ya kibinadamu wa nchini Marekani anasema kuhusiana na mgongano mkubwa uliopo katika siasa za Marekani kuhusu suala la haki za binadamu: "....Haki za binadamu za Kimarekani zinafungamana moja kwa moja na mapato ya mafuta na maslahi ya kifedha, hivyo madamu maslahi hayo ya Marekani yanadhaminiwa hapo huwa hakuna tena suala la kuheshimiwa haki za binadamu."

Kwa masikitiko makubwa, taasisi na mashirika ya kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa, yamekuwa yakinyamazia kimya jinai za wazi zinazotekelezwa na utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina na vilevile jinai za utawala wa Saudia dhidi ya watu wa Yemen kutokana na ushawishi mkubwa wa Marekani katika mashirika hayo.

Inasikitisha kuona kwamba mwenendo huo wa ukiukwahi wa wazi wa haki za binadamu ungali unaendelea kukaririwa na madamu undumakuwili huo utadumishwa, haki za binadamu zitaendelea kukanyagwa na kupuuzwa kutokana na tamaa za kisiasa na maslahi haramu ya madola makubwa duniani. Ni wazi kuwa siasa hizo za kibaguzi kuhusiana na suala la haki za binadamu zitapelekea jamii ya kimataifa kutoziamini tena taasisi na mashirika ya kimataifa yaliyopewa jukumu la kusimamia na kulinda haki za binadamu duniani, ambayo kwa sasa yanadhibitiwa na nchi za Magharibi na hasa Marekani.

Pamoja na hayo, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni moja ya nchi muhimu zinazoshirikiana kwa karibu na mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani na kuzungumzia wazi wazi udharura wa kulindwa haki hizo katika asasi za kimataifa bila kumwogopa yeyote. Ni kwa kuzingatia suala hilo ndipo ikatoa taarifa kuhusiana na kukandamizwa na maafisa wa usalama, washiriki wa  maaandamano ambayo yamekuwa yakifanyika kila siku ya Jumamosi huko Ufaransa katika miezi ya hivi karibuni na kulitaka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa pamoja na katibu mkuu wake, watoe ripoti maalumu zinazohusiana na ukandamizaji huo na kuipasha habari vilivyo jamii ya kimataifa kuhusu kadhia hiyo.

Kama alivyosema Muhammad Jawad Larijani, Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu ya Vyombo vya Mahakama vya Iran, katika kikao hicho cha mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kigeni wanaoishi humu nchini, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetaka kuwasilisha fikra yake kuhusiana na suala zima la sheria miongoni mwa wataalamu wa masuala ya sheria wa nchi tofauti, mbali kabisa na masuala ya kisiasa.



/129