Main Title

source : Pars Today
Jumatano

26 Juni 2019

08:59:45
955229

Kuzinduliwa mpango wa Dola bilioni 50 unaohusiana na Muamala wa Karne

Rais Donald Trump wa Marekani na katika fremu ya uungaji mkono wake wa kila upande kwa utawala khabithi wa Kizayuni, akiwa na Jared Kushner mkwe na mshauri wake wa karibu, amebuni mpango unaoitwa 'Muamala wa Karne' kwa ajili ya kuanzisha kile kinachodaiwa kuwa ni amani kati ya Wapalestina na Wazayuni.

(ABNA24.com) Rais Donald Trump wa Marekani na katika fremu ya uungaji mkono wake wa kila upande kwa utawala khabithi wa Kizayuni, akiwa na Jared Kushner mkwe na mshauri wake wa karibu, amebuni mpango unaoitwa 'Muamala wa Karne' kwa ajili ya kuanzisha kile kinachodaiwa kuwa ni amani kati ya Wapalestina na Wazayuni.

Katika uwanja huo sambamba na kukaribia tarehe ya kufanyika mkutano wa kiuchumi wa mjini Manama, Bahrain na ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezwaji wa mpango huo, ikulu ya Marekani (White House) imezindua mpango wa kiasi cha Dola bilioni 50. Trump amesema kuwa, mgogoro wa Israel na Palestina ni mgogoro mgumu zaidi duniani na kwamba kama kuna njia bora zaidi ya kuutatua, basi ni 'Muamala wa Karne.' Kwa mujibu wa vipengee vya mpango huo wenye kurasa 40 ambao umechapishwa katika mtandao wa ikulu ya Marekani, uwekezaji katika nyuga za kijamii na sekta binafsi katika ardhi za Palestina utaibua kwa akali fursa za ajira milioni moja. Kadhalika mpango huo unasema kuwa, kutakuwa na uwekezaji wa kiasi cha Dola bilioni 27.5 katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza, na kiasi cha Dola bilioni 9.1, Dola bilioni 7.4 na Dola bilioni 6.3 kwa utaratibu huo kwa ajili ya Wapalestina wanaoishi Misri, Jordan na Lebanon. Kwa mujibu wa mpango huo, White House inadai kwamba: "Vizazi kadhaa vya Wapalestina vimeishi katika mazingira magumu yenye matatizo, lakini katika kipindi kinachokuja wataweza kuishi kwa uhuru na katika mazingira mazuri zaidi."

Inaendela kudai kwamba mpango huo ndiyo hatua muhimu zaidi ambayo imewahi kuchukuliwa kimataifa kwa ajili ya Wapalestina kufikia sasa. Inafaa kuashiria kuwa katika miezi ya hivi karibuni, viongozi wa serikali ya Trump wamethibitisha kwamba, katika mkutano wao wa fursa za kiuchumi mjini Manama, mji mkuu wa Bahrain, kutazinduliwa pia hatua ya kwanza ya kiuchumi ya Muamala wa Karne. Kongamano la Manama limepangwa kufanyika kati ya tarehe 25 na 26 za mwezi huu nchini Bahrain. Katika miaka ya hivi karibuni utawala wa Aal-Khalifa umeimarisha sana uhusiano wake na utawala haramu wa Kizayuni. Hata hivyo kutangazwa mpango wa kiasi cha Dola bilioni 50, kumekabiliwa na radiamali hasi kutoka kwa Wapalestina. Katika uwanja huo, Hanan Ashrawi, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO ameuelezea mpango huo kuwa ni moja ya ahadi zisizotekelezeka na kuongeza kwamba, ni njia ya kisiasa tu ndiyo inayoweza kuhitimisha mzozo wa Israel na Palestina. Aidha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) sambamba na kukosoa vikali mpango huo imetangaza kwamba, Palestina si ya kuuzwa. Hazim Qassim, Msemaji wa harakati hiyo amesema: "Kwa mara nyingine tena serikali ya Marekani imekumbwa na njozi na inadhani kwamba raia wa Palestina watakubali kuamiliana kuuza haki yao mkabala wa fedha."

Kwa mujibu wa Muamala wa Karne, mji wa Quds utakuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni, huku maeneo makubwa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan yakikabidhiwa Wazayuni sambamba na kufutwa haki ya kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika ardhi zao asilia. Hata Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambayo hadi sasa imeshafanya maridhiano chungu nzima na utawala haramu wa Kizayuni, imeutaja mpango huo kuwa usiokubalika. Kwa kuzingatia kuwa mpango wa Muamala wa Karne unakinzana na mapendekezo ya Umoja wa Mataifa na wanachama wengine wa pande nne, yaani Umoja wa Ulaya na China, kuhusiana na namna ya utatuzi wa kadhia ya Palestina, hivyo mpango huo umepingwa pia na wanachama hao. Pamoja na hayo bado serikali ya Rais Donald Trump katika fremu ya kutekeleza hatua ya kwanza ya Muamala wa Karne katika mkutano wa mjini Manama, inaendelea kukusanya fedha zinazohitajika kutoka kwa nchi na pande zitakazoshiriki mkutano huo, ili iweze kufanikisha mpango huo. Hadi sasa Marekani imezishinikiza nchi nyingi za Kiarabu na Kiislamu kwa ajili ya kuzilazimisha zikubali kushiriki mkutano huo wa Bahrain. Akizungumzia mkutano huo, Mike Pompeo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema: "Ni matumaini yetu kwamba nchi za Kiarabu zitashiriki mkutano huo ili angalau zipate kusikia yatakayosemwa huko." Aidha ameongeza kwamba, hatarajii kwamba washiriki baada ya mkutano huo wataendelea kuutetea mpango wa Marekani. Kwa utaratibu huo hata Pompeo mwenyewe tayari ameonyesha kutokuwa na matumaini ya nchi za Kiarabu kuukaribisha mkutano huo.




/129