Main Title

source : Pars Today
Jumatatu

1 Julai 2019

02:43:45
956459

Uungaji mkono wa moja kwa moja wa nchi saba za Ulaya kwa JCPOA na kupigwa hatua ya kivitendo

Umoja wa Ulaya na troika ya Ulaya inayozijumuisha nchi za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kama wanachama wa kundi la 4+1, mara kwa mara zimekuwa zikitangaza uungaji mkono wao kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

(ABNA24.com) Umoja wa Ulaya na troika ya Ulaya inayozijumuisha nchi za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kama wanachama wa kundi la 4+1, mara kwa mara zimekuwa zikitangaza uungaji mkono wao kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Katika mabadiliko ya hivi karibuni kabisa katika uwanja huo, nchi kadhaa za Ulaya sambamba na kuunga mkono mapatano hayo zimesisitiza kwamba Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zitashirikiana na Iran kwa ajili ya kurahisisha mabadilishano ya kibiashara na Tehran. Austria, Ubelgiji, Finland, Uholanzi, Slovenia, Sweden na Uhispania nazo pia sambamba na kutoa taarifa ya pamoja juu ya ulazima wa kulindwa mapatano hayo, zimesisitiza kwamba JCPOA ni kadhia muhimu kwa ajili ya kudhibiti silaha na nguzo kuu ya kulindwa usalama na utulivu wa eneo la Asia Magharibi. Taarifa iliyotolewa na nchi hizo imesema: "Kwa kuzingatia kuwa utekelezwaji wa vipengee vya kiuchumi vya makubaliano hayo umekumbwa na matatizo, sisi tutashirikiana na Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na taasisi nyingine na kamisheni ya Ulaya kwa ajili ya kubuni njia inayorahisisha mabadilishano ya kifedha na Iran." Aidha nchi hizo zimesisitiza kwamba moja ya hatua za kwanza za kiuvumbuzi ni kuanzishwa mfumo maalumu wa kusahilisha mabadilishano ya kibiashara ya pande mbili au kwa jina jingine INSTEX.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba  kwa kuzingatia kuzinduliwa mfumo huo, ni muhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iendelee kufungamana na ahadi zake katika mapatano ya JCPOA. Hii ni katika hali ambayo Uholanzi pia  inakusudia kuongezwa katika orodha ya nchi zilizojiunga na mfumo huo wa kifedha. Kwa utaratibu huo idadi ya nchi ambazo zinataka kujiunga na mfumo huo wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zitaongezeka. Inaonekana kwamba hatua ya malalamiko ya Iran ikiwemo ya kupunguza kiwango cha ahadi zake katika mapatano ya JCPOA na pia indhari yake kali kuhusu uwezekano wa kujiondoa kikamilifu katika makubaliano hayo ya kimataifa iwapo haitodhaminiwa mahitaji yake ya kisheria, ndio imezisukuma nchi saba zilizotajwa kutoa taarifa hiyo ya pamoja. Harakati za nchi za Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa kifedha wa INSTEX na uungaji mkono wa nchi nyingine za Ulaya kwa mfumo huo ziliongezeka tangu Tehran ilipowasilisha malalamiko yake kwa Umoja wa Ulaya ikitaka kudhaminiwa maslahi yake ya kiuchumi kupitia mapatano ya JCPOA na kwamba kama nchi hizo hazingechukua hatua basi Iran ingepunguza ahadi zake katika makubaliano hayo. Itakumbukwa kuwa baada ya Marekani kujiondoa kwenye mapatano hayo ya nyuklia, tarehe 8 Mei mwaka jana, nchi wanachama wa Ulaya katika mapatano tajwa na troika ya EU zilitangaza kuwa ili kukabiliana na athari hasi za vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran, zingeendelea kushirikiana kibiashara na Tehran sambamba na kuanzisha mfumo maalumu wa kifedha kati ya pande mbili unaoitwa INSTEX kwa ajii ya shughuli hiyo.

Pamoja na hayo, kabla ya Iran kutoa muhula wa siku 60 kwa nchi hizo za Ulaya, nchi hizo zilikuwa hazijachukua hatua yoyote ya maana katika uga huo. Mwishoni mwa kikao cha kamisheni ya pamoja ya JCPOA mjini Vienna, Austria siku ya Ijumaa vyombo vya habari viliripoti habari ya EU kuanza kutekeleza ahadi zake. Naye kwa upande wake Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kisiasa alisema katika kikao hicho: "Miamala kupitia mfumo wa kifedha wa INSTEX imeanza kufanya kazi. Tumekubaliana na pande nyingine kufanyike kikao cha mapema cha ngazi ya mawaziri." Pamoja na hayo Araqchi alisisitiza kuwa: "Sidhani kama kumefikiwa maendeleo ya kutosha ya kuifanya Iran ibadili msimamo wake kuhusiana na kupunguza kiwango cha ushirikiano wake katika mapatano ya nyuklia." Kwa upande wake Helga Schmid, Naibu Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya pia alisisitizia kuanza kufanya kazi mfumo huo wa mabadilishano ya kifedha wa INSTEX. Akielezea suala hilo alisema: "Kufikia sasa INSTEX inafanya kazi na hatua ya kwanza ya mabadilishano inaendelea kutekelezwa na pia wanachama wengi wa Umoja wa Ulaya wanataka kujiunga na mfumo huo. Kuhusu miradi ya amani ya nyuklia ya Arak na Fordo pia maendeleo mazuri yamefikiwa."  Aidha Umoja wa Ulaya ulitoa taarifa baada ya kumalizika kikao hicho cha Vienna kwamba, ukisema kuwa mfumo wa kifedha wa INSTEX kati ya umoja huo na Iran umeanza kufanya kazi. Nayo Russia kama mmoja wa wanachama wa kundi la 4+1 imesisitizia kutoshirikiana na nchi nyingine katika kuiwekea vikwazo Iran. Kwa mujibu wa Moscow, hatua ya kuanza kutekelezwa ahadi za Umoja wa Ulaya kuhusiana na INSTEX kwa ajili ya kushirikiana na Iran kibishara ni hatua moja mbele kwa ajili ya kusimama imara dhidi ya hatua za kibabe za Marekani katika uga wa kimataifa hususan dhidi ya Iran.




/219