Main Title

source : Pars Today
Jumatano

3 Julai 2019

08:57:33
957507

Hatua mpya ya Iran katika kujibu ukiukaji ahadi wa madola ya Ulaya; Iran yavuka kiwango cha kilo 300 za urani iliyorutubishwa

Kwa mujibu wa kifungu nambari 36 cha makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, Iran imevuka kiwango cha kilo 300 za urani iliyorutubishwa.

(ABNA24.com) Kwa mujibu wa kifungu nambari 36 cha makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, Iran imevuka kiwango cha kilo 300 za urani iliyorutubishwa.

Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliashiria ukiukaji ahadi wa madola ya Ulaya katika kutekeleza makubaliano ya JCPOA pamoja na hatua mpya ya Iran alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu ya juzi na kusema kuwa, Iran ilitangaza wazi na bayana kabisa kwamba, inapunguza ahadi na uwajibikkaji wake katika makubaliano hayo ya kimataifa ya nyuklia. 

Dakta Zarif alisema wazi kuwa, katika hatua inayofuata ya kupunguza ahadi ilizojifunga nazo Iran kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Tehran itavuka kiwango cha kilo 300 za urani iliyorutubishwa kwa asilimia 3.67. Uamuzi wa Iran wa kuongeza akiba ya urani umefanyika kwa mujibu wa vipengee vya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na wala hatua hiyo haihesabiwi kwamba, ni ukiukaji wa makubaliano yenyewe. 

Kazem Gharib Abadi, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika asasi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna Austria, Jumatatu iliyopita aliashiria ripoti ya 15 ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomikia (IAEA) kuhusiana na kufungamana Iran na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kwamba: Hatua ya Iran ya kujitwalia haki zake inachukuliwa kwa mujibu wa vifungu nambari 26 na 36 vya makuabaliano ya nyuklia ya JCPOA. Kwa muktadha huo, kuanzia Mei mwaka huu Iran ilichukua hatua za kupunguza baadhi ya ahadi ilizotoa kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Kupunguzwa na Iran baadhi ya ahadi na uwajibikaji wake na kuanza kufanyika baadhi ya shughuli za miradi ya nyuklia ambazo zilikuwa zimesitishwa katika fremu ya makubaliano ya nyukliia, ni hatua ya kwanza ya jibu la Iran kwa kujiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia na vilevile kutoa majibu kwa madola ya Ulaya ambayo yamekuwa hayatekezi ahadi zake zilioahidi kwa Iran kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Filihali, hatua iliyochukuliwa na Iran kuhusiana na akiba ya maji mazito na urani iliyorutubishwa inatuma ujumbe muhimu kwa ukiukaji ahadi madola yaliyofikia makubaliano ya nyuklia na Iran. Baadhi wanaamini kwamba, katika mazingira ya sasa Iran imefungwa mikono na miguu. Hii ni katika hali ambayo, hatua hiyo ya Iran ni sehemu moja tu ya hatua nyingi zinazoweza kuchukuliwa na Tehran.

Sabah Zanganeh, mtaalamu wa masuala ya kimataifa anasema kuwa: Madhali Iran ingali inafanya mambo katika mkondo wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ina haki ya kustafidi na uwezo uliopo na hivyo kuweka kando uwajibikaji wake wa ziada katika makubaliano hayo. Kwa muktadha huo, hakutakuweko na ukiukaji wowote wa asili ya makubaliano ya nyuklia. 

Kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA kiwango cha urani iliyorutubishwa  ambayo inapaswa kuweko ndani ya Iran ni kilo 300 na itakayozidi inapaswa kupelekwa katika nchi nyingine. Lakinii Marekani kwa kuiwekea vikwazo Iran inataka makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yakumbwe na mkwamo. Hatua hii ya Marekani inafuatilia malengo mawili makuu:

Mosi, kuilazimisha Iran isimamishe kikamilifu urutubishaji wa madini ya urani, lengo ambalo limekwishagonga ukuta na kushindwa. Lengo la pili ni mwenendo wa kuzusha uongo na propaganda mpya kwamba, eti Iran imekiuka makubaliano ya nyuklia. Hii ni katika hali ambayo, hatua za Iran zinakwenda sambamba na kikamilifu kabisa na vifungu vya makubaliano ya JCPOA.

Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran anasema kuwa, kwa mujibu wa JCPOA, sisi ni lazima tukiuze au kukibadilisha kiwango kitakachozidi baada ya tani 130 za maji mazito au ziada ya kilo 300 ya urani iliyorutubishwa; lakini Marekani imetangaza kuwa, hakuna mtu mwenye haki ya kununua bidhaa hizo kutoka Iran kwa sababu Washington inataka uzalishaji huu usimamishwe. Sisi pia kwa kuwa tunafungamana na JCPOA endapo tutashindwa kuuza kile kitakachozidi baada ya tani 130 za maji mazito au ziada ya kilo 300 za urani iliyorutubiishwa tutakuwa hatuna budi ghairi ya kusimamisha uzalishaji. Katika hatua mpya, sisi hatufungamani na mpaka wa kuzalisha na kuuza na tunachotaka ni kuweka akiba baada ya kuzalisha. Thamani ya stratejia ya akiba ni hii kwamba, kuweko hayo hapa nchini pasina mpaka.

Hivi sasa ambapo fursa ya siku 60 iliyotolewa na Iran kwa madola ya Ulaya haijabakia isipokuwa siku chache tu, kutangazwa akiba ya urani iliyorutubishwa ya Iran ya kuvuka kiwango cha kilo 300, ni indhari kubwa kwa pande zilizobakia katika makubaliano hayo. Baada ya Marekani kujiondoa katika JCPOA Mei mwaka jana na Iran kutekeleza kifungo cha 36, madola ya Ulaya yalitoa ahadi 11 ambapo hayajatekeleza hata moja.

Hii ni katika hali ambayo, hata mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya (INSTEX) si katika ahadi hizo 11, bali huu ni utangulizi tu wa kutekkelezwa ahadi hizo.

Kwa kuzingatiia mazingira haya, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, endapo madola ya Ulaya yatachukua hatua za lazima kwa ajili ya kutekeleza ahadi na uwajibikaji wao kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA, basi Tehran inaweza kusitisha hatua ilizochukua. Lakini kama hayatafanya hivyo, Iran itapunguza uwajibikaji wake kwa mujibu wa kifungo cha 36 cha JCPOA.



/129