Main Title

source : Pars Today
Jumanne

30 Julai 2019

09:59:34
965846

Kesi ya Sheikh Zakzaky yaakhirishwa hadi Agosti 5, mawakili wataka aachiwe huru kwa ajili ya matibabu

Mahakama ya Nigeria leo imeakhirisha kikao cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa kwa ajili ya kumwachia huru kwa dhamana kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo IMN, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye wafuasi wake wasiopungua 20 waliuawa juma lililopita wakiandamana kwa amani ili kuishinikiza serikali imwachie huru.

(ABNA24.com) Mahakama ya Nigeria leo imeakhirisha kikao cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa kwa ajili ya kumwachia huru kwa dhamana kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo IMN, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye wafuasi wake wasiopungua 20 waliuawa juma lililopita wakiandamana kwa amani ili kuishinikiza serikali imwachie huru.

Mahakama ya mji wa kaskazini mwa Nigeria wa Kaduna imeakhirisha kesi hiyo hii leo hadi tarehe 5 mwezi ujao wa Agosti.

Mawakili wa mwanazuoni huyo wameitaka mahakama imwachie huru kwa ajili ya matibabu kutokana na hali yake mbaya ya kiafya. Madaktari wanasema Sheikh Zakzaky amepoteza jicho lake moja kutokana na mateso na kwamba jicho lake la pili pia huwenda likaharibika iwapo hatapata matibabu haraka iwezekanavyo.   

Mapema leo polisi ya Nigeria ilikuwa imeimarisha usalama huku wafuasi wa Sheikh Zakzaky waliokuwa wamekusanyika mbele ya mahakama wakitarajiwa kufanya maandamano ya kushinikiza aachiliwe huru.

Mahakama ya jimbo la Kaduna ilitazamiwa kusikiliza kesi hiyo hii leo Jumatatu na kutoa uamuzi iwapo itamwachilia huru kwa dhamana kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) kwa ajili ya kupatiwa matibabu au la.

Kiongozi huyo ambaye amekuwa kizuizini tangu Disemba 2015 anasemekana kupewa sumu akiwa kizuizini na anahitajia matibabu ya dharura nje ya nchi ili kuokoa maisha yake. Hayo ni kwa mujibu wa wanachama wa harakati hiyo ya Kiislamu.

Wafuasi wa harakati hiyo wamekuwa wakiandamana mara kwa mara katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja wakishinikiza kuachiliwa kwake kwa mujibu wa hukumu ya mahakama, lakini polisi na askari usalama wa nchi hiyo wamekuwa wakikabiliana nao kwa mkono wa chuma.

Siku chache kabla ya kusikilizwa kesi hiyo, Mahakama Kuu ya Federali katika mji mkuu Abuja iliiruhusu serikali kuitaja Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) kuwa ni kundi la kigaidi.

Kwa mujibu wa msemaji wa harakati hiyo, askari usalama wa Nigeria waliwaua wanachama 20 wa harakati hiyo katika maandamano yaliyofanyika siku ya Ijumaa.

Shirika la Haki za Binadamu la Kiislamu la mjini London Uingereza, limelaani mauaji yanayofanywa na askari usalama wa Nigeria dhidi ya Waislamu wa harakayti hiyo na kuitaka serikali ya Abuja isimamishe mauaji hayo mara moja

Wakati huohuo, waungaji mkono wa Sheikh Zakzaky wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa Nigeria mjini London wakitaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru mara moja.

Jana Jumapili Ofisi ya Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ilipiga marufuku shughuli za Harakati ya Kiislamu ya Nigeria IMN ikiituhumu kuwa ni kundi la kigaidi.



/129