Main Title

source : Pars Today
Jumapili

4 Agosti 2019

09:22:45
966827

Serikali ya Nigeria yakataa ombi la kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky na kuletwa Iran kwa ajili ya matibabu

Serikali ya Nigeria imekataa ombi la Iran la kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kisha aletwe hapa nchini kwa ajili ya matibabu.

(ABNA24.com) Serikali ya Nigeria imekataa ombi la Iran la kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kisha aletwe hapa nchini kwa ajili ya matibabu.

Taarifa iliyochapishwa jana Jumamosi na gazeti moja la nchi hiyo likizinukuu duru za ndani ya serikali ya Abuja inasema kuwa, serikali ya nchi hiyo imepinga ombi la Iran la kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky na kisha aruhusiwe kuja hapa nchini kwa ajili ya matibabu.

Taarifa ya serikali ya Nigeria imeeleza kwamba, kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky na kisha kuruhusiwa asafiri kwenda Iran kwa ajili ya matibabu kutatatiza usalama wa Nigeria katika mustakabali.

Aidha taarifa hiyo imedai kwamba, hata kama Sheikh Zakzaky ataachiliwa huru, katu hataruhusiwa kusafiri nje ya nchi, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumpatia fursa ya kujizatiti tena kwa silaha.

Hivi karibuni Sheikh Muhammad Jafar Montazeri, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwaandikia barua viongozi wa mahakama nchini Nigeria ambapo sambamba na kutoa wito wa kuungwa mkono haki za Sheikh Ibrahim Zakzaky aliwataka wamuachilie huru mwanaharakati huyo na kisha waruhusu asafiri na kuja kutibiwa hapa nchini Iran.

Sheikh Zakzaky na mkewe walipigwa risasi na tangu wakati huo wanashikiliwa katika korokoro za serikali ya Rais Muhammadu Buhari ambayo inaendelea kukaidi amri ya Mahakama Kuu ya kumwachilia huru mwanachuoni huyo.



/129