Main Title

source : Pars Today
Jumanne

6 Agosti 2019

09:40:50
967372

Mahakama ya Kaduna Nigeria yatoa hukumu ya kuachiliwa Sheikh Zakzaky kwa ajili ya matibabu

Mahakama Kuu ya Kaduna nchini Nigeria leo imetoa hukumu ya kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu yay Nigeria na kuruhusiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

(ABNA24.com) Mahakama Kuu ya Kaduna nchini Nigeria leo imetoa hukumu ya kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu yay Nigeria na kuruhusiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Mahakama ya jimbo la Kaduna ambayo leo imesikiliza ombi la kuachiliwa huru kwa dhamana Sheikh Ibrahim Zakzaky imetoa hukumu ya kuachiliwa huru mwanaharakati huyo pamoja na mkewe na kwenda kupatiwa matibabu nje ya nchi.

Aidha taarifa iliyotolewa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imeeleza kwamba, kiongozi wao huyo sasa anaruhusa yeye pamoja na mkewe ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwa mujibu wa harakat hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe mara baada ya kuachiliwa huru wanatarajiwa kusafiri na kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu.

Akisoma hukumu hiyo leo, hakimu wa jalada la kesi hiyo amesema kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wanapaswa kuachiliwa na kwenda kutibiwa nje ya nchi kwani hali yao ya kiafya si nzuri.

Hivi karibuni, Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna iliwaachilia huru wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky hatua ambayo ilileta matumaini ya kufutiwa mashataka pia mwanaharakati huyo wa Kiislamu.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alikamatwa baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya yeye na mke wake mwezi Disemba 2015 wakati jeshi la nchi hiyo lilipovamia Husseiniya ya Baqiyyatullah mjini Zaria na kuua kkwa umati mamia ya Waislamu.



/129