Main Title

source : Pars Today
Jumamosi

17 Agosti 2019

08:15:20
969413

Sheikh Zakzaky: Nigeria imeipotosha India kuhusiana na hali yangu ya kiafya

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, serikali ya Abuja imeipatia India taarifa za uongo kuhusiana na hali yangu ya kiafya hatua ambayo imekwamisha mwenendo wa matibabu yake.

(ABNA24.com) Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, serikali ya Abuja imeipatia India taarifa za uongo kuhusiana na hali yangu ya kiafya hatua ambayo imekwamisha mwenendo wa matibabu yake.

Sheikh Zakzaky amesema hayo katika mkanda wa vidio ambapo amesisitiza kwamba, kutokana na mazingira yalivyo hivi sasa anafadhilisha kuondoka nchini India na kwenda nchi nyingine kwa ajili ya kkufuatilia matibabu yake.

Akizungumza katika mkanda huo wa video, Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, kutokana na ukwamishaji mambo katika mwenendo wa matibabu yake uliofanywa na serikali ya Nigeria  anaona bora arejee nchini kwake na kisha kuangalia uwezeklano wa kwenda nchi nyingine kwa ajili ya matibabu.

Mwanaharakati huyo wa Kiislamu ambaye kwa muda mrefu sasa hali yake ya kiafya imezorota amesema kuwa, madaktari wa India wamemueleza kwamba, hawana taarifa yoyote kuhusiana na maradhi anayosumbuliwa nayo au faili lake la kitiba ili waanze matibabu; hivyo ni lazima aanze kufanyiwa vipimo upya.

Kwa mujibu wa Sheikh Zakzaky, madkatari wa India hata hawana taarifa kama ana risasi mwilini.

Mawakili wanaomtetea kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wanasema kuwa, jicho la kulia la Sheikh Zakzaky limepoteza nguvu za kuona na kuna uwezekano jicho lake jingine likapata tatizo kama hilo.

Sheikh Ibrahim Zakzaky aliwasili New Delhi nchini India Jumatatu iliyopita kwa ajili ya matibabu, baada ya Mahakama Kuu ya Kaduna kutoa idhini ya mwanaharakati huyo wa Kiislamu kwenda kutibiwa nje ya nchi.



/129