Main Title

source : Pars Today
Jumamosi

17 Agosti 2019

08:30:25
969420

Serikali ya Nigeria inajaribu kumuua Sheikh Zakzaky

Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imetangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo inajaribu kumuua kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.

(ABNA24.com) Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria imetangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo inajaribu kumuua kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Taarifa iliyotolewa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria siku ya Alhamisi imesema: "Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Nigeria wa kumpa idhini Sheikh Zakzaky na mkewe kusafiri India kupata matibabu ulikuwa kinyume na takwa la serikali ya Nigeria."

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imesisitiza kuwa, serikali ya Nigeria imekuwa ikijaribu kutumia kila mbinu kumuua Sheikh Zakzaky na hatimaye kuiangamiza harakati hiyo ili kuandaa mazingira ya kurejea kikamilifu satwa ya mabeberu wa Magharibi katika nchi hiyo ya Afrika.

Aidha taarifa hiyo imesema iwapo Sheikh Zakzaky atapewa matibabu chini ya usimamizi wa madaktari wake binafsi nchini Nigeria, basi kutafichuka kasfha kubwa na kwa msingi huo utawala wa Nigeria umekuwa ukimuwekea mwanazuoni huyo vizingiti katika matibabu yake.

Sheikh Zakzaki jana Alhamisi alilazimika kuondoka New Delhi India alikokuwa amefika siku chache zilizopita kupata matibabu. Sheikh Zakzaky ameachukua uamuzi huo kutokana na kutoridhika na mchakato mzima wa matibabu pamoja na vizingiti vya usalama alivyowekewa sambamba na kunyimwa ruhusha madakatari wake anaowaamini kumtibu. Sheikh Zakzaky anatazamiwa kuwasili mjini Abuja Nigeria baadaye hivi leo. Kwa mujibu wa Masoud Shajareh wa Kituo cha Haki za Binadamu za Kiislamu chenye makao yake mjini Laondon, Sheikh Zakzaky hakupata matibabu yoyote yanayofaa nchini India.

Ikumbukwe kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe walitiwa nguvuni na askari wa jeshi la Nigeria Desemba 13, 2015 katika shambulio na uvamizi uliofanywa na askari hao dhidi ya Huseiniya ya mji wa Zaria nchini humo.

Siku hiyo askari wa jeshi la Nigeria waliwafyatulia risasi watu waliokuwa wamejumuika kwenye kituo hicho cha kidini na mbele ya nyumba ya msomi huyo na kuwaua shahidi mamia miongoni mwao wakiwemo watoto wake watatu wa  kiume. Sheikh Zakzaky pamoja na mke wake walijeruhiwa vibaya sana katika tukio hilo na wiki hii hatimaye utawala wa Nigeria uliwaruhusu kupata matibabu.



/129