Main Title

source : Pars Today
Jumatano

21 Agosti 2019

09:30:13
970284

Waislamu waandamana Abuja, Nigeria wakitaka kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky

Waislamu katika mji wa Abuja nchini Nigeria wameandamana wakitaka kuachwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.

(ABNA24.com) Waislamu katika mji wa Abuja nchini Nigeria wameandamana wakitaka kuachwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.

Televisheni ya Euro News imeripoti kuwa, mamia ya wakazi wa mji wa Abuja jana waliandamana wakipiga nara za kuachiwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba picha za Sheikh Zakzaky, wameitaka serikali ya Rais Muhammadu Buhari kumuachia huru mwanazuoni huyo wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, kwa sasa Sheikh Zakzaky anashikiliwa mahala kusikojulikana na kwamba, tangu aliporejea kutoka India alichukuliwa na vyombo vya usalama na kupelekwa kusikojulikana.

Hivi karibuni, Ibrahim Musa, msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alisema kuwa, harakati hiyo inavitaka vyombo vya usalama vya nchi hiyo vinavyomshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky kuutangazia umma mahala vinapomshikilia kiongozi huyo wa Kiislamu.

Alkhamisi iliyopita Sheikh Zakzaky alilazimika kuondoka New Delhi India alikokuwa amefika siku chache kabla kupata matibabu. Sheikh Zakzaky alichukua uamuzi huo kutokana na kutoridhika na mchakato mzima wa matibabu pamoja na vizingiti vya usalama alivyowekewa sambamba na kunyimwa ruhusa madakatari wake anaowaamini kumtibu.  

Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe walitiwa nguvuni na askari wa jeshi la Nigeria Desemba 13, 2015 katika shambulio na uvamizi uliofanywa na askari hao dhidi ya Huseiniya ya mji wa Zaria nchini humo.



/129