Main Title

source : Pars Today
Jumatano

21 Agosti 2019

09:53:01
970295

Serikali ya Nigeria yaendeleza njama dhidi ya kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini humo

Askari usalama wa Nigeria wameendeleza vitimbi na njama zao dhidi ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky na kumpeleka mahala pasipojulikana.

(ABNA24.com) Askari usalama wa Nigeria wameendeleza vitimbi na njama zao dhidi ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky na kumpeleka mahala pasipojulikana.

Tarehe 12 Agosti Sheikh Zakzaky na mkewe walipelekwa India kwa ajili ya matibabu lakini walirejeshwa Nigeria tarehe 15 mwezi huu wa Agosti kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa matibabu yao, vikwazo na mbinyo wa kiusalama na kutokuwepo madaktari anaowaamini yeye.

Taarifa iliyotolewa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inasema, baada kuwasili katika uwanja wa ndege wa Abuja, askari usalama wa Nigeria walimkamata tena Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe na kuwapeleka mahala pasipojulikana bila hata ya kuwapa waandishi habari waliokuwa wakisubiri kwa muda mrefu fursa ya kuzungumza naye.

Japokuwa Waislamu wa Nigeria wamekuwa chini ya mbinyo na mashinikizo ya askari usalama wa serikali ya nchi hiyo kwa miaka mingi lakini mashinikizo hayo yameongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni hususan baada ya kutiwa nguvuni Sheikh Ibrahim Zakzaky katika shambulizi la kinyama lililolenga kituo cha Kiislamu cha Baqiyatullah hapo mwaka 2015 katika mji wa Zaria. Mamia ya Waislamu waliuawa kinyama katika shambulizi hilo wakiwemo watoto watatu wa Sheikh Zakzaky. Serikali ya Nigeria pia imepiga marufuku mikutano na mikusanyiko ya aina yoyote ya wafuasi wa mwanazuoni huyo.

Ushahidi unaonesha kuwa, chanzo cha mbinyo na mashinikizo hayo yote dhidi ya wanaharakati wa Kiislamu wa Nigeria hususan Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky ni ushawishi wa Marekani, Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel katika siasa za nchi hiyo. Mwenendo wa matukio ya kisiasa ya miaka ya hivi karibuni katika nchi kama Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel unaonesha kuwa, baada ya kushindwa kwa siasa za tawala hizo katika kanda ya Mashariki ya Kati, viongozi wa tawala hizo wameamua kupanua zaidi ushawishi wao barani Afrika, na katika uwanja huo Nigeria ambayo inahesabiwa kuwa na utajiri mkubwa wa nishati na maliasili na yenye jamii kubwa zaidi ya watu barani Afrika, inapewa umuhimu maalumu. Kwa msingi huo viongozi wa tawala hizo wanafanya jitihada kubwa za kutaka kuwa na satua na ushawishi mkubwa zaidi katika misimamo ya serikali ya Nigeria hususan viongozi wa ngazi za juu na maafisa wa jeshi kwa kutumia njia ya misaada ya kifedha na zana za kivita na kuwapambanisha na Waislamu hususan wanaharakati miongoni mwao.

Haroun Nahiroha ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu anasema: "Kundi la mawahabi ndiyo sababu kuu ya mashinikizo na mbinyo mkubwa unaowasumbua Waislamu wa Nigeria hususan Waislamu wa madhehebu ya Shia. Wasaudia wanaihimiza serikali ya Abuja izuie kasi kubwa ya kuenea na kupanuka madhehebu ya Shia nchini humo kwa sababu hakuna mrengo mwingine wenye mvuto na vuguvugu kubwa la Kiislamu nchini Nigeria kama walivyo Waislamu wa madhehebu hiyo; hivyo serikali ina wasiwasi mkubwa kuhusiana na suala hilo."

Uchochezi wa Saudia, Marekani na Israel na woga huo wa harakati za Waislamu hususan wafuasi wa Ahlulbait ndiyo sababu kuu za mbinyo na ukandamizaji unaoshuhudiwa hivi sasa dhidi ya wanaharakati wa Kiislamu hususan Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye wameamua kummaliza kabisa kimwili au kisiasa. Ni katika fremu hiyo ndiyo maana safari ya kitiba ya Sheikh Zakzaky nchini India iliyofanyika baada ya miezi kadhaa ya malalamiko ya jumuiya za kutetea haki za binadamu, ikakatizwa bila hata ya kupewa matibabu kutokana na mashinikizo ya serikali ya Abuja. Mwanazuoni huyo ambaye amekamatwa tena na vyombo vya dola baada tu ya kuwasili katika uwanj wa ndege wa Abuja, amepelekwa kusikojulikana licha ya hali yake mbaya ya kiafya. Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imetangaza kuwa, serikali ya Abuja inatumia mbinu mbalimbali kumuua Sheikh Zakzaky na kuangamiza harakati yake. Kabla ya hapo pia vyombo vya usalama vya Nigeria vilikuwa vimetangaza kuwa, Serikali ya Federali ya nchi hiyo imewasilisha tuhuma mpya dhidi ya Sheikh Zakzaky na kwamba kuna uwezekano akapigwa marufuku kutoka nje ya nchi.

Ingawa Waislamu na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanaendelea kufanya juhudi za kuhakikisha Sheikh Ibrahim Zakzaky anaruhusiwa kwenda nje ya Nigeria kwa ajili ya kupata matibabu lakini inaonekana kuwa, serikali ya Abuja imeazimia kuendelea kupuuza sheria za kimataifa na haki za binadamu na kummaliza kabisa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo. Hata hivyo serikali ya Abuja imeghafilika na ukweli kwamba, kummaliza Sheikh Ibrahim Zakzaky hakutaweza kufuta au kusimamisha mkondo wa harakati ya Kiislamu na wapigania uhuru na haki nchini Nigeria.   






/129