Main Title

source : Pars Today
Jumatatu

23 Septemba 2019

06:06:03
977408

Kumbukumbu ya kuanza vita vya kulazimishwa, maonyesho ya uwezo wa kijeshi wa Iran

Tarehe 31 Sharivar sawa na tarehe 22 Septemba, inasadifiana na kuanza vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran.

(ABNA24.com) Miaka 39 iliyopita katika siku kama ya leo, jeshi vamizi la utawala wa Saddam (dikteta wa zamani wa Iraq) kwa msaada wa Marekani na kwa uungaji mkono wa kifedha wa Saudia na Kuwait, lilianzisha mashambulizi makali dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hatimaye vita hivyo vilifikia tamati kwa kushindwa na kudhalilika muungano wa maadui baada ya kupita miaka minane, na kwa kuibuka na ushindi na izza taifa la Iran. Vita vya kulazimishwa vilivyojumuisha matatizo mengi na mashinikizo dhidi ya nchi hii, vilibadilika na kuwa tajriba yenye thamani kubwa ya kusimama kidete taifa la Iran. Mafanikio hayo makubwa ni tukio la kubakia milele katika historia ya Iran, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Wakati ambao taifa la Iran linaadhimisha wiki ya kujihami kutakatifu kwa kukumbuka miaka minane ya kusimama imara mkabala wa hujuma za maadui, vikosi vya ulinzi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuanzia jeshi la kawaida, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), jeshi la kujitolea (Basiji) na jeshi la polisi, vimesimama imara kwa nguvu zake zote katika kukabiliana na pande zinazotishia usalama na uthabiti wa nchi hii. Akiwahutubia makamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Iran Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kuwa, kipindi cha kujihami kutakatifu ni dhihirisho la utukufu wa taifa la Iran na kusisitiza kuwa: "Pamoja na kwamba gharama za kimada na kimaanawi katika vita vya kulazimishwa zilikuwa kubwa, lakini mafanikio ya taifa la Iran katika miaka minane ya kujihami kutakatifu ni makubwa zaidi kuliko gharama....Tajriba ya miaka minane ya kujihami kutakatifu inaonyesha kwamba licha ya mibinyo na mashinikizo na kutokuwepo fedha za kutosha pamoja na matatizo mengine mengi, lakini ni jambo linalowezekana kukabiliana na mabeberu, na pia kusimama imara mbele ya tamaa za madola ya kiistikbari."

Kwa mtazamo wa uwezo wa kuzuia hujuma na hata wa mashambulizi, Iran inao uwezo wa kusimama imara kukabiliana na pande zinazovuruga usalama wa eneo. Katika uwanja huo, makombora yaliyotengenezwa na wataalamu wa humu nchini, yanahesabiwa kuwa moja ya nguzo za uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika uwanja huo, Jumamosi ya jana mjini Tehran katika marasimu ya ufunguzi wa maonyesho ya kwanza ya ndege zisizo na rubani za Marekani zilizotunguliwa na kuchukuliwa ngawira na jeshi la Iran, Hossein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) alisema: "Nchi yoyote itakayoishambulia kijeshi Iran, yenyewe itageuzwa kuwa uwanja wa vita." Naye kwa upande wake Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa kikosi cha anga na anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: "Hii leo na baada ya miaka 40 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na katika uwanja wa vitisho mbalimbali vya maadui, taifa la Iran limezidi kupata maendeleo tofauti yakiwemo ya kiulinzi na kijeshi." Kwa sasa Iran inatambuliwa kuwa moja ya nchi nne zenye uwezo mkubwa wa makombora duniani. Kuhusiana na suala hilo Maksim Shevchenko, mkuu wa kituo cha utafiti wa masuala ya Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) cha Russia anaelezea uwezo wa kiulinzi wa Iran kwa kusema: "Iran ina uwezo mkubwa zaidi wa kijeshi katika eneo la Asia Magharibi. Na vikosi vya kijeshi vya nchi hii vimefanikiwa kuzalisha aina tofauti za silaha za kisasa ambazo tumekuwa tukizishuhudia katika maonyesho tofauti ya jeshi la Iran."

Ni suala lililo wazi kwamba kwa kuzingatia uwezo huo, adui yeyote atalazimika kufanya mahesabu makali kabla ya kufikiria kufanya shambulizi lolote dhidi ya Iran hasa kutokana na uwezo wa kiulinzi na wa mashambulizi wa nchi hii, ili kwa njia hiyo adui huyo aweze kufahamu gharama na faida zitakazotokana na uvamizi wowote dhidi ya Iran. Katika kujadili uwezo wa kijeshi wa Iran kuna nukta muhimu kadhaa: Mosi ni kwamba, nafasi ya kistratijia ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kulinda usalama na kukabiliana na vitisho, ni suala muhimu sana. Pili ni kuingia jeshi la Iran katika hatua ya kutekeleza nafasi ya kistratijia katika ngazi ya kujilinda. Ngazi hiyo ina nafasi kubwa katika kulinda usalama na uthabiti wa eneo. Kamwe Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kufuatilia malengo ya kuibua vita katika eneo, lakini haitofumbia macho suala la kukabiliana na adui na vitisho.



/129