Main Title

source : ParsToday
Jumanne

24 Desemba 2019

07:57:00
996079

Ripoti: Sheikh Zakzaky na mkewe wanakabiliwa na hali mbaya gerezani

Ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetangaza kuwa, kiongozi huyo pamoja na mkewe Malama Zeenat wanakabiliwa na hali mbaya katika gereza wanaloshikiliwa.

(ABNA24.com) Taarifa hiyo imeeleza kuwa, zikiwa zimepita siku 18 tangu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat wahamishiwe katika gereza moja la serikali, hali yao ya kiafya ni mbaya kutokana na mazingira mabaya ya sehemu wanaposhikiliwa.

Aidha taarifa hiyo imebainisha kwamba, wawili hao hawapati huduma za awali kabisa za kimsingi kama dawa na matibabu na hivyo kutishia usalama wa maisha yao.

Baadhi ya ripoti kutoka zinasema kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria yuko katika hali mbaya sana ya kiafya gerezani na anaugua magonjwa kadhaa bali yuko katika hali mahututi, jambo ambalo limezusha wasi wasi mkubwa.

Hivi karibuni Nasser Umar Safir daktari wa Sheikh Ibrahim Zakzaky alisema kuwa, msomi huyo ameathiriwa na sumu na anapaswa kupewa matibabu haraka iwezekanavyo na kwamba, kuendelea kuwepo hai Sheikh Zakzaky licha ya hali yake mbaya ya kiafya ni jambo linalofanana na muujiza.

Sheikh Ibrahim Zakzaky(66), na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia na kushambulia kituo cha kidini cha Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi.

..........
340