Main Title

source : ParsToday
Jumatano

25 Desemba 2019

08:11:33
996347

Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt: Sheikh Zakzaky anapigania umoja wa Waislamu duniani

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt amesema kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky ni shakhsia anayepigania umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

(ABNA24.com) Ayatullah Reza Ramezani amesema hayo jana Jumanne katika kikao na waandishi wa habari, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka minne, tangu lijiri tukio la wanajeshi wa Nigeria kushambulia kituo cha kidini cha Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. jimboni Kaduna kaskazini mwa Nigeria.

Amebainisha kuwa, "Sheikh Zakzaky anapinga uhasama wa kimadhehebu miongoni mwa Waislamu, na ana anaamini kuwa mazungumzo ndiyo njia bora ya kuimarisha mshikamano."

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt ameongeza kuwa, sambamba na kukosoa hatua ya kuendelea kuzuilia kinyume cha sheria Sheikh Zakzaky, ameeleza bayana kuwa, mwanaharakati huyo wa Kiislamu wa Nigeria anaamini kuwa, taasisi anazozifanyia kazi zinawasaidia mayatima na masikini.

Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, Jumuiya ya Wahadhariri wa Vyuo Vikuu vya Kidini katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran ililaani hatua ya serikali ya Nigeria ya kumfunga jela kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria huku ikitoa mwito wa kuachiwa huru mwanazuoni huyo na kupewa matibabu haraka iwezekanavyo.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, (66) na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussaynia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, Waislamu wasiopungua 1,000, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi.

...........
340