Main Title

source : ParsToday
Jumapili

29 Desemba 2019

07:44:45
997190

Ripoti ya X-Ray: Kuna vipande 43 vya mabaki ya risasi kwenye mwili wa Zakzaky

Huku tahadhari juu ya hali mbaya ya kiafya ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky zikiendelea kutolewa; duru za hospitali zimefichua kuwa, vipande vya mabaki ya risasi vimekwama kwenye mwili wa mwahanarakati huyo wa Kiislamu.

(ABNA24.com) Majibu ya vipimo vipya vya miale ya X-Ray yanaonesha kuwa, "Kuna vipande 43 vya marisau ya risasi ambavyo vimekwama katika upande wa kushoto wa mwili wa Zakzaky." Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Sheikh Zakzaky anahitaji matibabu ya dharura.

Famili ya Sheikh Zakzaky imesema kwenye taarifa kuwa, "Kama inavyoonekana kwenye picha za miale ya X-Ray, moja ya risasi za wanajeshi magaidi liliharibu kikamilifu jicho la Sheikh Zakzaky na kumpofusha."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, makatili wa Kiwahabbi waliolipwa na utawala wa Saudia walifanya juu chini kuhakikisha kuwa wanamuua Sheikh Zakzaky. Historia bila shaka itarekodi upeo wa juu wa ukatili wa Mawahabbi.

Hivi karibuni pia, Daktari wa Sheikh Zakzaky, Nasser Umar Safir alisema kuendelea kuwepo hai mwanaharakati huyo wa Kiislamu licha ya hali yake mbaya ya kiafya ni jambo linalofanana na muujiza.

Alisema kuwa, baada ya kuchunguza mwili na afya ya Sheikh Zakzaky imebainika kuwa, ameathiriwa na kemikali na sumu iliyotokana na zana na vyombo vinavyotumiwa katika jela ya Kaduna.

Itakumbukwa kuwa tarehe 13 Disemba 2015, jeshi la Nigeria lilifanya mauaji ya kikatili dhidi ya Waislamu wa Nigeria baada ya kuivamia Husainia ya mji wa Zaria, mbali na kumteka nyara Sheikh Zakzaky baada ya kumpiga risasi kadhaa.

..........
340