Main Title

source : ParsToday
Ijumaa

3 Januari 2020

13:23:19
998807

Muhammad Zarif: Kuuawa shahidi Soleimani kutaimarisha zaidi mapambano ya Kiislamu kieneo na kimataifa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika shambulio la kigaidi lililotekelezwa na Marekani mapema leo Ijumaa, kutaimarisha zaidi mti wa mapambano ya Kiislamu katika eneo na ulimwengu mzima kwa ujumla.

(ABNA24.com) Meja Jenerali Qassim Soleimani, ameuawa leo Ujumaa alfajiri nje ya uwanja wa ndege wa Baghdad katika shambulio la anga la askari vamizi na wa kigaidi wa Marekani. Huku akilaani vikali shambulio hilo la kigaidi, Muhammad Jawad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwa kusema: Ukhabithi na upumbavu wa askari wa kigaidi wa Marekani katika kumuua shahidi Meja Jenarali Soleimani, shahidi shupavu na jenerali mwanapambano dhidi ya ugaidi na fikra za upindukiaji mipaka, bila shaka utaimarisha zaidi mti wa mapambano katika eneo na ilimwengu mzima.

Zarif ameongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatumia uwezo wake wote wa kisiasa, kisheria na kimataifa kwa ajili ya kutekeleza maamuzi ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa ili kuuwajibisha utawala wa kijinai na kigaidi wa Marekani kuhusiana na jinai hiyo ya wazi.

Zarif pia ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba Marekani itabeba dhima ya matokeo yote yatakayotokana na chokochoko zake zilizo kinyume cha sheria katika eneo.

Amesisitiza kwamba nafasi ya Marekani katika ugaidi wa kimataifa na mauaji ya kigaidi dhidi ya Meja Jenerali Suleimani, ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika kuwaangamiza magaidi wa Daesh, an-Nusra, al-Qaida na makundi mengine ya kigaidi ni jambo hatari sana linalozidisha mvutano wa kipumbavu katika eneo.

...........
340