Main Title

source : ParsToday
Ijumaa

3 Januari 2020

13:23:19
998808

Joe Biden ambaye ni miongoni ma wanasiasa wa chama cha Democratic wanaochuana kupata tiketi ya kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao wa rais utakaofanyika mwaka huu nchini Marekani amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa kutoa amri ya kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Meja Jenerali Qassem Soleimani.

(ABNA24.com) Joe Biden ametoa taarifa akisema taarifa ya serikali ya Donald Trump imedai kuwa lengo la mauaji hayo ni kuzuia mashambulizi tarajiwa ya Iran, lakini hatua hiyo yenyewe itakuwa na matokeo kinyume chake.

Biden amemtaka Donald Trump awaeleze wananchi wa Marekani stratijia yake ya kulinda wanajeshi wa Marekani walioko Asia Mashariki.

Mapema leo Ijumaa Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani.

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. 

...........
340