Main Title

source : ParsToday
Ijumaa

3 Januari 2020

13:23:19
998809

Bei za mafuta na dhahabu katika soko la kimataifa kote duniani zimepanda kufuatia kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran, Meja Jenerali Qassem Soleimani.

(ABNA24.com) Duru za habari zinaarifu kuwa, bei ya mafuta katika soko la kimataifa leo Ijumaa imeongezeka kwa dola mbili kwa pipa. Aidha ugaidi huo wa kimataifa wa Marekani umepelekea kuongezeka kwa bei ya dhahabu duniani, mbali na kuporomoka kwa masoko ya hisa ya nchi za Ulaya kwa angalau asilimia 0.5.

Jeffrey Halley, mchambuzi wa uchumi wa Asia Pasikifiki amesema bei ya dhahabu imeongezeka kwa asilimia 1 na kufikia dola 1,543.66 na kwamba bei hiyo inatazamiwa kuongezeka ndani ya siku chache zijazo hadi dola 1,575, kutokana na taharuki iliyoibuliwa na Marekani kufuatia mauaji ya Jenerali Soleimani.

Nchi nyingi duniani zikiwemo China, Russia, Iraq na Lebanon zimeonya kuhusu matokeo mabaya ya ugaidi huo wa kiserikali wa utawala wa Washington.

Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani. 

...........
340