Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

4 Januari 2020

08:24:06
999146

Balozi wa Iran UN: Jibu la mauaji ya kigaidi ya Jenerali Soleimani litakuwa la hatua ya kijeshi

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, jibu la mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani yaliyofanywa na Marekani bila shaka litakuwa la hatua ya kijeshi.

(ABNA24.com) Majid Takht-Ravanchi ametoa sisitizo hilo katika mahojiano maalumu na kanali ya televisheni ya CNN ya Marekani na akaongeza kuwa, Marekani imechukua hatua ya kijeshi ya kumuua shahidi mmoja wa makamanda waandamizi wa Iran, kwa hivyo inapasa tusubiri kushuhudia ni vipi, lini na mahala gani jibu la jinai hilo litatolewa na Iran.

Akijibu suali alioulizwa la kama anaiona hatua ya Marekani kuwa ni kilelezo cha vita, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, ukweli ni kwamba mauaji ya kigaidi ya Jenerali Qassem Soleimani ni hatua ya vita ambayo imeanzishwa na Marekani dhidi ya wananchi wa Iran.

Takht-Ravanchi ameongeza kuwa: Kwa hatua iliyochukua usiku wa kuamkia Ijumaa, ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Soleimani, Marekani imefungua ukurasa mpya, ambao ni wa kuanzisha vita dhidi ya Iran.

Akijibu suali kwamba kauli ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei kuhusu "kisasi kikali kinachowangojea watenda jinai" na kwamba kwa kuwa watu hao si wengine ila ni Marekani, je huko si kutangaza vita?, Takht-Ravanchi amesema, tangu muda mrefu nyuma Marekani imshaanzisha vita dhidi ya Iran.

Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu haiwezi kufumbia macho kilichotokea na hakuna shaka yoyote italipiza kisasi, na kisasi chenyewe kitakuwa kikali.

.........
340