Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

4 Januari 2020

08:24:07
999148

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na mashahidi wengine katika jinai ya Marekani Ijumaa asubuhi mjini Baghdad na kusisitiza kuhusu kulipiza kisasi kufuatia jinai hiyo.

(ABNA24.com) Katika taarifa siku ya Ijumaa, IRGC imelaani hujuma ya angani ya vikosi vamizi na vya kigaidi vya Marekani ambayo imelenga gari lililokuwa limembeba Meja Jenerali Soleimani, wenzake na makamanda wa Harakati ya Al Hashd al Shaabi ya Iraq akiwemo mpigana jihadi mkubwa, Abu Mahdi al Muhandes ambaye alikuwa akitekeleza mpango wa kukabiliana na njama mpya ya Marekani ya kuhuisha ISIS na makundi mengine ya magaidi wakufurishaji sambamba na kuvuruga tena usalama wa Iraq. Taarifa hiyo imesema waliouawa shahidi  wamepata fahari kubwa.

IRGC imesisitiza kuhusu kuendeleza njia ya mashahidi na kuongeza kuwa, Meja Jenerali Suleimani hakuwa tu shakhsia bali alikuwa ni fikra kamili na kuanzia sasa maadui wataweza kushuhudia upeo mkubwa zaidi wa fikra hizo katika maeneo ambayo wameeneza satwa yao kinyume cha sheria duniani.

Taarifa hiyo aidha imesisitiza kuwa Meja Jenerali Suleimani na wengine ambao wamelelewa katika fikra za Utawala wa Faqihi na Mapambano ya Kiislamu, wamefungua ukurasa mpya katika mapambano na muqawama dhidi ya Wazayuni na katika kukabiliana na magaidi pamoja na Wamarekani wavamizi katika eneo.

Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema jana Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ametoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani. 

.........
340