Main Title

source : ParsToday
Jumapili

5 Januari 2020

08:13:13
999428

Dakta Zarif: Uingiliaji wa vikosi vya kigeni ndio sababu ya kuongezeka mivutano katika eneo

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran haitaki kuona kunakuweko mivutano katika eneo la Asia Magharibi na kusisitiza kwamba, uwepo wa vikosi vya kigeni na vya nje ya eneo hili ndio sababu ya ukosefu wa amani na usalama na chimbuko la kuongezeka migogoro katika eneo hili.

(ABNA24.com) Dakta Muhammad Javad Zarif amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar.

Zarif ameitaja hatua ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassiim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) kuwa ni ya kigaidi na kueleza kwamba, Marekani itabeba dhima ya matokeo ya jinai hiyo.

Kwa upande wake Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar ameitaja hali ya Asia Magharibi katika mazingira ya sasa hasa baada ya tukio la jana la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) kuwa ni nyeti na ya kutia wasiwasi na kusisitiza kwamba, kuna haja ya kupatikana ufumbuzi wa amani kwa ajili ya kupunguza mivutano na migogoro.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliofanya mazungumzo yao alasiri ya leo hapa mjinii Tehran wamebadilishana mawazo pia kuhusiana na masuala ya pande mbili pamoja na matukio muhimu ya kieneo na kimataifa. 

.........
340