Main Title

source : ParsToday
Jumapili

5 Januari 2020

08:13:14
999429

Kamisheni ya Bunge: Marekani itarajie kisasi kikali kwa hatua yake ya kumuua Qassim Soleimani

Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa, Marekani mtenda jinai isubirie kisasi kikali dhidi yake kutokana na hatua yake ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH).

(ABNA24.com) Taarifa ya Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani vikali mauaji hayo ya kinyama ya Marekani imeeleza bayana kwamba, Marekani, utawala haramu wa Israel na ubeberu wa dunia watambue kwamba, kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani kutazidi kupelekea umoja na mshikamano wa mhimili wa muqawama na kuzidi kuleta hofu na woga ya kudumu kwa Wamarekani.

Aidha taarifa ya Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa, chombo hicho kitafanya tathmini na uchunguzi wa kina na kukabidhii ripoti yake kwa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, viongozi, shakhsia, taasisi na jumuiya mbalimbali za kieneo na kimataifa zimeendelea kulaani jinai ya jana ya Marekani dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema jana Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

..........
340