Main Title

source : ParsToday
Jumapili

5 Januari 2020

08:13:18
999430

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na Naibu Mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al-Hashdul al-Shaabi, Abu Mahdi al-Muhandes kutapelekea kuimarika zaidi ari na moyo wa mapambano.

(ABNA24.com) Sheikh Zakzaky amesema katika taarifa aliyoyotoa na kueleza kwamba, anatoa mkono wa pole na tanzia kwa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Marajii Taklidi na Waislamu kote duniani hususan familia za mashahidi hawa mashujaa.

Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema pia katika taarifa hiyo kwamba, kwa mara nyingine tena mabeberu wamechukua hatua ya kichochezi kwa kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes

Sehemu nyingine ya taarifa ya Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imesema kuwa, jinai hiyo ya Marekani katu haitapunguza hata chembe juhudi za wanamapambano za kuhuduumia Uislamu.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Wakazi wa mji mkuu wa Nigeria, Abuja wamefanya maandamanao ya kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Meja Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH wakati akiwa safarini nchini Iraq.

Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu wa mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hashdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

...........
340