Main Title

source : ParsToday
Jumapili

5 Januari 2020

08:14:39
999431

Umati mkubwa wausindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani mjini Baghdad

Umati mkubwa wa watu umejitokeza leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliyeuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

(ABNA24.com) Waombolezaji walioshiriki katika shughuli hiyo wakiwa wamebeba picha za mashahidi Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes pamoja na bendera za Harakati ya Hashd al-Shaabi na Brigedi ya Hizbullah ya Iraq walisikika wakipiga nara za mauti kwa Marekani.

Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa Iraq alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki katika shughuli hiyo ya kuuaga na kuusindikiza mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani.

Aidha waombolezaji hao wameonyesha chuki zao dhidi ya hatua za Marekani, Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel huko Iraq.

Baada ya mwili wa shahidi Qassim Soleimani kuagwa katika mji wa Kadhmein, ulipelekwa Karbala na baadaye Najaf, ambapo baadaye ulitarajiwa kuletwa hapa nchini.

Baada ya mwili wa shahidi Qassim Soleimani kuwasili hapa nchini utapelekwa Mash'had ambapo kesho Jumapili kutafanyika shughuli ya kuuaga katika haram ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (as).

Taarifa zaidi zinasema kuwa, siku ya Jumatatu wananchi wa Tehran watapata fursa ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi huyu mwanamapambano ambaye anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne katika kijiji chao katika mji wa Kerman.

............
340