Main Title

source : ParsToday
Jumapili

5 Januari 2020

09:08:38
999441

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa mpangaji wa mikakati iliyopoelekea Marekani ipate hasara za kistratijia na kuongeza kuwa: "Kuuawa kigaidi Jenerali Suleimani ni mwanzo wa kumalizika uwepo wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi."

(ABNA24.com) Meja Jenerali Hussein Salami, Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) akizungumza na mwandishi wa IRIB kufuatia kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC amesisitiza kuwa: "Bila shaka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu litachukua hatua kali ya kulipiza kisasi na Marekani itajuta."

Meja Jenerali Salami ameendelea kusema kuwa Luteni Jenerali Soleimani amechora mistari katika eneo kubwa la kijiografia na kuunda nguvu ambayo imepelekea kushindwa magaidi wakufurishaji na hasa ISIS au Daesh ambao walianzishwa na Marekani.

Kamanda wa IRGC amesema kuendelea utambulisho wa pamoja wa makundi ya muqawama au mapambano ya Kiislamu kunatokana na jitihada za kijihadi za Luteni Jenerali Qassem Suleimani na kuongeza kuwa, ni wazi kuwa maadui hawangeweza kustahamili uwepo wa kamanda kama huyo na hatimaye wametekeleza kitendo cha kumuua shahidi.

Aidha kamanda mkuu wa IRGC ametoa onyo kwa waitifaki wa utawala wa Marekani, ambao ni adui wa umma wa Kiislamu, na kusema wanapaswa kusitisha njama zao ili wasiwe waathirika wa sera za Washington.

Kamanda Mkuu wa IRGC amesema mrengo wa muqawama na mapambano ya Kiislamu una azma imara ya kuendeleza mapambano yenye malengo matakatifu sambamba na kulipiza kisasi damu iliyomwagwa kidhulma ya makamanda wake ambao wameuawa shahidi. Meja Jenerali Salami amesema mustakabali utakuwa mwema kwani kumalizika uwepo wa Marekani ni jambo ambalo litaleta  uthabiti, ustawi, usalama na mlingano katika eneo la Asia Magharibi.

..........
340