Main Title

source : ParsToday
Jumapili

5 Januari 2020

09:08:39
999443

Taathira za kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis

Usiku wa manane wa kuamkia juzi Ijumaa Januari 3 viongozi wa Marekani walitekeleza kitendo cha kijinai na kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (Hashdu al Shaabi).

(ABNA24.com) Swali muhimu linaloulizwa hapa ni, jinai hiyo itakuwa na taathira na matokeo gani?

Taathira ya kwanza ni kwamba, jinai hiyo imekuwa sababu ya kuongezeka mshikamano na umoja wa kitaifa ndani ya jamii ya Iran.

Wananchi wa Iran wanamtambua Luteni Jenerali Qassem Soleimani kuwa ni shakhsia mzalendo na wa kipekee. Ndio maana tangu juzi Ijumaa wananchi na shakhsia mbalimbali wa Iran kwa mshikamano na sauti moja wamelaani na kuyataja mauaji hayo ya Soleimani kuwa ni  jinai.

Taathira ya pili ya jinai hiyo ni kuwa, umoja kati ya Iraq na Iran umeongezeka sasa. Viongozi wa Marekani miezi miwili iliyopita wamefanya juhudi na njama kubwa za kuibua hitilafu na mgawanyiko kati ya nchi mbili za Iran na Iraq, hata hivyo kushiriki pakubwa na kwa wingi wananchi wa Iraq katika shughuli ya kusindikiza na kuaga miili ya mashahidi Soleimani na al Muhandes kumedhihirisha kuwa, jinai hiyo ya Marekani imezidisha umoja kati ya Tehran na Baghdad.

Taathira ya tatu ya jinai hiyo ni kwamba, ghadhabu na hasira dhidi ya Marekani zimeongezeka khususan miongoni mwa wananchi wa Iraq.

Wananchi wa Iraq ambao jana Jumamosi walishiriki kwenye shughuli ya kuaga na kusindikiza miili ya mashahidi hao walikuwa wakipiga nara kwa sautii moja za "Mauti kwa Marekani" na kutaka wanajeshi wa Marekani waondoke huko Iraq.  

Taathira ya nne ni kwamba jinai hiyo imebadilisha mitazamo ya wananchi wa Iran kuhusu Marekani. Ervand Abrahamian Mhadhiri wa Vyuo Vikuu nchini Marekani ambaye pia ni mchambuzi mtajika wa masuala ya Iran anazungumzia jambo hilo akisema: Wairani hadi sasa walikuwa wakiitambua Marekani kama serikali inayopanga njama, hata hivyo sasa wananchi hawa wanaitambua Marekani kama serikali ya kigaidi  baada ya kumuua Qassem Soleimani.  

Taathira ya tano ya jinai hiyo imekuwa ni kuzidisha na kuimarisha azma ya mhimili wa muqawama ili kuboresha nafasi yake. Viongozi wa Marekani wanaendesha propaganda kubwa ikiwa ni katika jitihada za kudhihirisha kuwa kitendo cha kumuua kigaidi Luteni jenerali Qassem Soleimani ni ushindi mkubwa kwao kwa sababu wamemuua mmoja wa makamanda wa mhimili wa muqawama.

Hata kama Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa mmoja wa makamanda muhimu wa mhimili wa muqawama na kama alivyomtaja Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwamba alikuwa "Shakshsia wa Kimataifa wa Muqawama", lakini kosa inalofanya Marekani ni kuichukulia nguvu na uwezo wa mhimili wa muqawama kuwa unategemea "mtu binafsi".

Ukweli ni kwamba mhimili wa muqawama umethibitisha kuwa haukusimama kwa kumtegemea mtu binafsi, kama ambavyo baada ya kuuliwa kigaidi Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Abbas Musawi, Sayyid Hassan Nasrullah alishika nafasi yake na leo hii yeye ni mmoja wa shakhsia muhimu zaidi na wenye uwezo mkubwa zaidi kiuongozi katika eneo la Asia Magharibi, kiasi cha kumtia kiwewe na hofu kubwa adui mzayuni.   

Na taathira ya sita ya jinai hiyo ni kuweza kuwa sababu ya kufukuzwa wanajeshi wa Marekani huko Iraq. Marekani imekiuka mamlaka ya kujitawala ya Iraq na kuamua kuwaua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandes Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea (Hashdu al Shaabi), ambaye pia ni mmoja wa makamanda muhimu wa Iraq.

Kwa msingi huo, juzi Ijumaa viongozi na shakhsia wa Kiiraqi pia wametaka rasmi kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini humo Iraq; na hata Ayatollah Haeri mmoja wa marajii taqlid wa Iraq pia ametoa fatwa akisema kuwa ni haramu wanajeshi wa Marekani kuweko huko Iraq.

..........
340